Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Julius Kalanga Laizer

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Monduli

Primary Question

MHE. JULIUS K. LAIZER aliuliza:- Tanzania ni nchi ya tatu (3) Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya takribani mifugo milioni 25 lakini sekta hii bado mchango wake katika pato la Taifa ni ndogo ukilinganisha na idadi ya mifugo tuliyonayo:- (a) Je, Serikali ina mkakati gani wa kujenga viwanda vya nyama, ngozi na maziwa hapa nchini ili kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na mifugo? (b) Je, ni lini Serikali itaanza kutoa ruzuku ya madawa kama Ndigana Kali, Homa ya Mapafu na dipu kwa wafugaji wetu nchini?

Supplementary Question 1

MHE. JULIUS K. LAIZER: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu ya Serikali, sekta hii ya mifugo bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwepo utitiri wa tozo mbalimbali kwa wafugaji ambao karibu ng’ombe moja tozo zake zinazidi shilingi elfu hamsini. Swali la kwanza, je, nini mkakati wa Serikali kuwapunguzia wafugaji tozo hizo ili waweze kuzalisha kwa tija?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, tatizo linalowakabili wafugaji wengi nchini ni pamoja na ugonjwa wa Ndigana Kali ambapo wafugaji tunapoteza zaidi ya asilimia 60 ya ndama wakati wanapozaliwa na chanjo hii bei yake ni shilingi 12,000 kwa ndama. Je, nini mkakati wa Serikali wa kuweka ruzuku au kuondoa kodi katika chanjo hii ili wafugaji waweze kumudu?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya mawili ya Mheshimiwa Laizer, Mbunge wa Monduli, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utitiri wa tozo, Wizara imeendelea na utaratibu wa kupitia tozo zote zinazotozwa katika sekta hii ya mifugo na zile zinazoonekana kuwa ni kero kwa wafugaji wetu na wafanyabiashara wa mifugo tumeendelea kuzipunguza. Vilevile zile ambazo zimeonekana kuwa ziko chini tumeendelea kuziongeza kwa manufaa mapana ya Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili anataka kujua kuhusiana na chanjo. Taasisi yetu ya TVLA na TVI mpaka sasa Tanzania sisi wenyewe tumefanikiwa kutengeneza chanjo tano na chanjo ya Ndigana Kali ni miongoni mwa chanjo tunayoifikiria kuiongezea. Naomba tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba jambo hili lipo katika mkakati wa Wizara na yenyewe itatengenezwa hapa Tanzania na tutakapofanikiwa itapunguza bei na kuwasaidia wafugaji wetu.

Name

Aysharose Ndogholi Mattembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JULIUS K. LAIZER aliuliza:- Tanzania ni nchi ya tatu (3) Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya takribani mifugo milioni 25 lakini sekta hii bado mchango wake katika pato la Taifa ni ndogo ukilinganisha na idadi ya mifugo tuliyonayo:- (a) Je, Serikali ina mkakati gani wa kujenga viwanda vya nyama, ngozi na maziwa hapa nchini ili kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na mifugo? (b) Je, ni lini Serikali itaanza kutoa ruzuku ya madawa kama Ndigana Kali, Homa ya Mapafu na dipu kwa wafugaji wetu nchini?

Supplementary Question 2

MHE. AISHAROSE N. MATEMBE: Nakushukuru Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Mkoa wa Singida kama ilivyo Monduli ni mabingwa wa kufuga ng’ombe, mbuzi na kondoo.

Je, Serikali ina mpango gani wa haraka wa kuanzisha kiwanda kikubwa cha ngozi na nyama ili kuendana na falsafa ya Tanzania ya Viwanda?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Aisharose Matembe, Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Singida juu ya kuanzishwa kiwanda cha kuchakata nyama na mazao ya mifugo katika Wilaya ya Manyoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoeleza katika jibu la msingi kwamba Serikali imekuwa na mkakati huo na maeneo mbalimbali katika Taifa letu hivi sasa viwanda vinajengwa. Wazo hili la kujenga pale Manyoni ni jema, naomba tulichukue tulipeleke kwa wawekezaji ili tuweze kupata kiwanda pale Manyoni ambako ni center kwa mifugo inayotoka katika Mkoa wa Kigoma na Mikoa ya Bara kwa maana ya Shinyanga na hata Nzega na Tabora wote wanaweza kupata huduma hii ya kuchakata mifugo kwenye eneo hili kwa kuwa eneo hili ni la kimkakati.