Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Richard Phillip Mbogo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nsimbo

Primary Question

MHE. RICHARD P. MBOGO (K.n.y JAMAL KASSIM ALI) aliuliza: Mwaka 2017, Umoja wa Afrika (AU) ulipitisha Azimio kwa nchi za Afrika la kuhakikisha kuwa nchi hizi zinavuna faida itokanayo na Demografia iliyopo kwa kuwekeza kwa vijana:- (a) Je, Serikali ya Tanzania imechukua hatua gani katika utekelezaji wa Azimio hilo? (b) Je, ni mafanikio gani yamepatikana kama nchi baada ya utekelezaji huo?

Supplementary Question 1

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri. Nina maswali mawili madogo ya nyongeza:

Mheshimiwa Spika, tunajua Muungano wa Kikanda au wa Kimataifa kama vile SADC una faida kubwa nzuri sana kwa vijana hususan kwenye kupata ujuzi pamoja na mafunzo. Je, huu mkutano uliopita hivi karibuni nini vijana watafaidika na SADC?

Mheshimiwa Spika, swali la pili kuna maazimio gani ambayo tayari yaliyopo aidha kwenye EU umoja mwingine wa Kimataifa ambayo yatasaidia vijana zaidi kwenye suala lile la mikopo?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Spika, kwanza kwenye Mkutano wa SADC uliomalizika hivi karibuni tuchukue fursa hii kuwashukuru sana Wakuu wote wa nchi pamoja na Mwenyekiti wetu wa SADC kwa azma na kauli yao thabiti ya kuhakikisha kwamba vijana wanashiriki katiak sekta ya uchumi wa viwanda.

Mheshimiwa Spika, katika Mkutano uliomalizika agenda kubwa ilikuwa ni kuwashirikisha vijana katika uchumi wa viwanda na kwa Tanzania vijana walipata fursa ya kutembelea na kuona fursa mbalimbali na kujifunza kupitia Mataifa mengine na tunaamini kabisa kupitia Mkutano huu liko jambo ambalo limeongezeka katika fikra za vijana hasa katika kwenda kuwekeza kwenye uchumi wa viwanda. Kwa hiyo ni Mkutano ambao ulikuwa na tija na vijana wamehamasika na tunaamini kutokea hapo vijana wengi zaidi watashiriki katika uchumi wa viwanda, moja kwa moja au isivyo moja kwa moja.

Mhehsimiwa Spika, swali lake la pili alitaka kujua Maazimio ya Kikanda kupitia AU. Katika Azimio la 601 la mwaka 2017 katika moja ya nguzo iliyosemwa ni uwezeshwaji wa vijana na Serikali ya Tanzania tunayafanya hayo kupitia Mifuko mbalimbali ya Uwezeshaji wa Vijana na kuwajengea vijana uwezo hasa katika kuwajengea ujuzi ili waweze kujiajiri na kuajiri vijana wengine.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo Serikali ya Awamu ya Tano inayafanya hayo kuzingatia maamuzi yaliyofikiwa na Wakuu wa nchi katika Umoja wa Afrika.