Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Conchesta Leonce Rwamlaza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CONCHESTER RWAMLAZA (K.n.y MHE. JOSEPH L. HAULE) aliuliza:- Aliyekuwa Waziri wa Maji, Mheshimiwa Eng, Isack Kamwelwe, alitembelea chanzo cha maji cha Sigaleti kilichopo Kata ya Ruaha ambacho kimepimwa na kuthibitishwa na Wataalam wa Idara ya Maji kwamba, kina maji mengi na salama na kinaweza kuhudumia ipasavyo Kata za Ruaha, Kidodi na Ruhembe. Na kwamba, zinatakiwa shilingi bilioni 2 ili maji hayo yaweze kupatikana kwenye kata hizo:- Je, Serikali ipo tayari kutenga kiasi cha fedha kwenye bajeti, ili kuokoa maisha ya wananchi zaidi ya 35,000?

Supplementary Question 1

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu ya Naibu Waziri, ninayo maswali mawili ya nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, sasa Serikali imetenga pesa kama ilivyo katika majibu ya msingi. Na kwa kuwa, tatizo la maji katika Kata zilizotajwa katika swali hilo ni ya muda mrefu. Je, Serikali inaji-commit vipi kwamba, huu mradi wa kuweka maji katika kata hizo utakamilika wakati gani?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili ni kwamba, kumekuwa na matatizo makubwa sana katika miradi ya maji katika nchi yetu na Serikali inaahidi kutoa pesa kwenye bajeti, lakini fedha haziendi kama inavyotarajiwa, lakini pia hata fedha zinazoenda zinatumika vibaya na kuifanya miradi hii isikamilike. Je, Serikali sasa inachukua hatua zipi kuhakikisha kwamba, hii miradi ya maji ambayo inapata fedha za Serikali inakamilika na fedha zinatumika ipasavyo?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, nataka nimfahamishe Mheshimiwa Mbunge kwanza sisi kama Serikali tumefanya jitihada kubwa sana pale Mikumi Mjini. Zaidi ya mradi wa milioni 974 tumeweza kutekeleza kupitia chanzo cha Madibira katika kuhakikisha wananchi wale wanapata huduma ya maji, lakini katika kuhakikisha tunatumia chanzo hiki cha Sigaleti sisi tunapitia usanifu kwa mara ya mwisho kabisa. Na ninataka nimhakikishie sisi kama Wizara ya Maji tutafanya jitihada kuhakikisha mradi huu tunauanza na kutekeleza katika kuhakikisha azma ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kumtua mwanamama ndoo kichwani inatimilika.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili; utekelezaji wa miradi ya maji unategemeana na fedha. Na sisi kama Serikali, Serikali inatupa fedha moja ya changamoto kubwa ilikuwa ni muundo, lakini kupitia Bunge lako Tukufu umetunga sheria katika kuhakikisha kwamba, tuna sheria Namba 5 ya Huduma ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira na Uanzishwaji wa Wakala wa Maji RUWASA. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge huu utakuwa muarobaini katika kuhakikisha usimamizi wa miradi ya maji na fedha, kwa maana ya wakandarasi katika kuhakikisha wanatekeleza miradi ya viwango na katika kuhakikisha tunatatua matatizo ya maji, ahsante sana.

Name

Miraji Jumanne Mtaturu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Mashariki

Primary Question

MHE. CONCHESTER RWAMLAZA (K.n.y MHE. JOSEPH L. HAULE) aliuliza:- Aliyekuwa Waziri wa Maji, Mheshimiwa Eng, Isack Kamwelwe, alitembelea chanzo cha maji cha Sigaleti kilichopo Kata ya Ruaha ambacho kimepimwa na kuthibitishwa na Wataalam wa Idara ya Maji kwamba, kina maji mengi na salama na kinaweza kuhudumia ipasavyo Kata za Ruaha, Kidodi na Ruhembe. Na kwamba, zinatakiwa shilingi bilioni 2 ili maji hayo yaweze kupatikana kwenye kata hizo:- Je, Serikali ipo tayari kutenga kiasi cha fedha kwenye bajeti, ili kuokoa maisha ya wananchi zaidi ya 35,000?

Supplementary Question 2

MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza nianze kumshukuru sana Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kunijalia kuingia kwenye Bunge lako Tukufu na kuweza kuwawakilisha ipasavyo Wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Ikungi pamoja na Jimbo la Singida Mashariki ni kama ambavyo swali la msingi lilivyouliza lina matatizo yanayofanana na jimbo lililoulizwa katika swali la msingi. Pamoja na matatizo hayo zimefanyika jitihada, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya kipenzi chetu Dkt. John Pombe Magufuli, wameshatuletea takribani bilioni 1 na milioni 500 kuchimba visima virefu 28.

Mheshimiwa Spika, sasa nimekuja hapa kuomba kwa kupitia Waziri, wako tayari, tumeshafanya tathmini ya kutosha tuweze kupata, maana kuchimba maji na kuyapata ni jambo moja na kutoka maji ni jambo la pili. Kwa hiyo, ninaomba Mheshimiwa Waziri anihakikishie kwamba, kupitia tathmini iliyofanyika na iko Wizarani tunahitaji jumla ya bilioni 2 ili tuweze kutengeneza miundombinu ya maji Wananchi wa Singida wapate maji. (Makofi)

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, awali ya yote kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge, kwanza namfahamu vizuri alikuwa Mkuu wa Wilaya, lakini nataka niwahakikishie wana-Singida Mashariki hili ni jembe wembe walitumie vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, katika kuhakikisha kwamba, tunatatua tatizo hili la maji tumeshafanya jitihada za uchimbaji. Nimuombe baada ya Bunge Saa saba tukutane tupange mikakati ya kwenda kutatua tatizo la maji kwa haraka kabisa. Ahsante sana. (Makofi)