Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Victor Kilasile Mwambalaswa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupa

Primary Question

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA (K.n.y. MHE. JANET Z. MBENE) aliuliza:- Uchomaji wa mkaa kwa kiasi kikubwa unatumia miti ya asili pamoja na mapori ya akiba, ukataji wa miti hauendi sambamba na upandaji wa miti na hii ina athari kubwa sana kwenye mazingira yetu ikiwemo kupungua kwa mvua na kukauka kwa vyanzo vya maji:- Je, ni lini Serikali itaanza kutoza ada kwa mkaa unaosafirishwa nchi za nje ili iweze kurejesha mazingira katika hali yake?

Supplementary Question 1

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru pamoja na majibu mazuri saa ya Mheshimiwa Naibu Waziri kuhusu swali hili nina maswali ya nyongeza mawili. La kwanza nimemsikia Mheshimiwa Naibu Waziri akiongelea charcoal briquettes bada la mkaa wa kawaida kutumia charcoal briquettes ambao utengenezaji wake sio lazima utumie miti unatumia majani ya miti, majani ya kawaida haya kuweza kutengeneza mkaa huo ambao una nguvu kuliko mkaa wa kawaida.

Je, ni lini Serikali itaanza kuhamasisha wananchi waaanze kuchoma charcoal briquettes badala ya kutumia miti kuchoma mkaa hilo la kwanza?

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili nimefurahishwa sana na majibu ya nyongeza ya Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana kwenye swali la nyongeza la swali namba 68 kuhusu kupanda mamilioni ya miti kwenye Mlima Kilimanjaro ili kuupunguzia climate stress huu Mlima Kilimanjaro.

Je, ni lini Serikali itaanza kampeni hiyo ya kupanda miti sio tu kwenye Mlima Kilimanjaro bali nchi nzima wananchi waanze kupanda miti? (Makofi)

Name

Mussa Azzan Zungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ilala

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Naibu Waziri kwa majibu mazuri kwa swali la pili mkakati unaandaliwa sasa hivi wa kupanda miti katika Wilaya zote na sasa sio kupanda miti tu, kupanda na kuitunza miti ili isije ikafa. Mara nyingi sana halmashauri wanahamasika kupanda miti lakini baada ya muda mfupi miti ile inakufa na tutaweka aina maalum ya miti kwa Wilaya ambayo itakayoweza kufaa kuna miti mingine haifai kwenye Wilaya mbalimbali, miti hii inapandwa kwa gharama kubwa na inakufa. Kwa hiyo, program kaguzi tutaanza tutashirikiana na halmashauri zote kuhakikisha miti inapandwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa letu, nchi yetu imebarikiwa kuwa na asilimia 39.9 kuwa ni misitu, misitu hii inapotea. Kuanzia mwaka 1990 mpaka 2010 tumeshapoteza takribani hekta milioni nane ya misitu na hii ni hatari kubwa sana kwa Watanzania tuhakikishe tuache kukata miti tutunze miti kama fursa ya kibiashara, tutumie miti badala ya kukata tuweke mazao ya nyuki. (Makofi)

Name

Rhoda Edward Kunchela

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Katavi

Primary Question

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA (K.n.y. MHE. JANET Z. MBENE) aliuliza:- Uchomaji wa mkaa kwa kiasi kikubwa unatumia miti ya asili pamoja na mapori ya akiba, ukataji wa miti hauendi sambamba na upandaji wa miti na hii ina athari kubwa sana kwenye mazingira yetu ikiwemo kupungua kwa mvua na kukauka kwa vyanzo vya maji:- Je, ni lini Serikali itaanza kutoza ada kwa mkaa unaosafirishwa nchi za nje ili iweze kurejesha mazingira katika hali yake?

Supplementary Question 2

MHE. RHODA E. KUNCHELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante halmashauri zimekuwa zikichukua hatua kali sana kwa hawa wafanyabishara wa mkaa hususani katika mikoa ya pembezoni.

Sasa nataka nifahamu mkakati wa Serikali pamoja na juhudi ambazo mnazifanya za kuhakikisha tunatunza mazingira na ukizingatia uuzaji wa gesi bado ni gharama kwa mwananchi ambaye hana kipato kikubwa. Serikali mna mkakati wa gani wa kuhakikisha haya matumizi ya gesi kwa bei ya chini yanaenda sambamba na kupunguza gharama za manunuzi ya mkaa? (Makofi)

Name

Mussa Azzan Zungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ilala

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa kuleta gesi wananchi watumie umeshanza. Napongeza Wizara ya Nishati Pardot Project imeshaanza na imeshaanza kuonesha gharama ni za chini na hivi karibuni Wizara ya Nishati itaanza mkakati kuhakikisha gesi tunapitisha katika nyumba zote Dar es Salaam na tukitoka Dar es Salaam tunakwenda mikoa mingine Iringa kwa Msigwa kule. (Makofi)