Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Salum Mwinyi Rehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Primary Question

MHE. SALUM MWINYI REHANI aliuliza:- (a) Je, ni lini Mamlaka ya Hali ya Hewa itakuwa inatoa taarifa sahihi na za wakati kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa nchini? (b) Je, ni lini Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa kushirikiana na Idara ya Earthy Warming watakuwa wanatoa taarifa za hali ya upatikanaji wa mvua na ukame ili kuwaepusha wakulima wengi kulima na kupata hasara kwa kukosa mvua wakati wao wanajua hali itakavyokuwa?

Supplementary Question 1

MHE. SALUM MWINYI REHANI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Kwa kuwa moja ya vitu ambavyo nchi hii inatakiwa kuwa navyo ni iwe inaelewa mambo mengi yanayohusiana na hali ya hewa kwa sababu tuna vifaa ambavyo vimeunganishwa na satellite duniani lakini kinachosikitisha ni kwamba mara nyingi matukio mengi ambayo yanatakiwa yatolewe kwa tahadhari, kwa mfano tuna tishio la nzige sasa hivi, lakini tuna tishio la kweleakwelea na viwavi jeshi, kwa hali ya hewa inavyoonesha na hali ya hewa ya mvua hicho kitu time yoyote kinaweza kutokea katika maeneo yetu. Sasa matatizo haya huwa yanatokea katika maeneo mengi na hakuna taarifa zinazotolewa. Je, ni lini Serikali itakuwa ina utaratibu wa kuweza kutujulisha kama nchi, yale matukio ya hatari kama haya yanavyoweza kutokea na kuweza kujilinda na kuwa tayari kuweza kukabiliana nayo?

Name

Eng. Atashasta Justus Nditiye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba tumekuwa tukiwasiliana na wenzetu duniani kwa kutumia taaluma ya satellite na ndiyo maana hivi karibuni Serikali imeendelea kuwekeza katika vifaa vya kisasa kwa Mamlaka ya Hali ya Hewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sakata la nzige na masakata mengine ambayo yanatokea huwa tunayaona na bahati nzuri huwa tunatoa taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Hata taarifa zinapokuja huwa zimeanzia kwanza Mamlaka ya Hali ya Hewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba taarifa huwa tunakuwa nazo na tunazitoa mapema kabla. Ni vyema niwashauri Waheshimiwa Wabunge kwamba kabla ya kufanya kitu chochote baada ya taarifa ya habari wawe na muda mzuri wa kuangalia taarifa za hali ya hewa ambazo huwa zinatolewa kwa usahihi kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.