Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maida Hamad Abdallah

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAIDA HAMAD ABDALLAH aliuliza:- Sheria ya NHIF inamtambua Mtumishi wa Umma ambaye amechangia kwa miaka 10 pale anapostaafu kuwa atahudumiwa na Mfuko yeye na mwenza wake hadi mwisho wa maisha yao:- Je, kwa nini Serikali isiweke utaratibu kama huo kwa Viongozi wa Umma?

Supplementary Question 1

MHE. MAIDA HAMAD ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa naipongeza Serikali kwa kuweza kuendelea kuwahudumia wananchi wake wawapo kazini na wale ambao wamestaafu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kwamba kuna mabadiliko ya utaratibu wa uchangiaji kutoka miaka 10 hadi
15 lakini bado baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wamekuwa wakiendelea kuchangia miaka 20 na kuendelea lakini wazazi wao hawajatambuliwa kuwa wafaidika wa mfuko huo na ukiangalia wamechangia fedha nyingi na muda wanaopata matatizo ni mdogo. Vilevile kuna baadhi ya Waheshimiwa Wabunge hawana watoto, mume wala mke. Je, Serikali inaweka utaratibu gani wa kisheria kuweza kuwatambua Waheshimiwa Wabunge katika kufaidika na Mfuko huo watakapokuwa wamestaafu? (Makofi)

Name

Dr. Faustine Engelbert Ndugulile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigamboni

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Maida, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, amegusia kuhusiana na Wabunge ambao wamekua wanachangia Mfuko huu na kwa nini Serikali isifanye mabadiliko ya sheria. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Waheshimiwa Wabunge ndiyo tunatunga sheria na hii sheria ambayo inahusu mafao yetu ni sisi wenyewe tunahusika. Pili, ni sisi wenyewe Wabunge ambao tunatengeneza Kanuni zetu za Uendeshaji wa Bunge letu. Kwa hiyo, hili suala wala siyo suala la Serikali ni la Bunge lenyewe kukaa na kuamua kupitia Kanuni zao na Tume ya Utumishi wa Bunge kuweka utaratibu wa mafao na haki stahiki katika masuala ya bima ya afya kwa Waheshimiwa Wabunge.