Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

Hon. Lucy Fidelis Owenya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kupata nafasi ya kuchangia. Matumizi ya mifuko ya plastic; ni jambo jema kwa Serikali kutoa tamko mwisho wa kutumia mifuko ya plastic ni 1/6/2019. Tamko pekee halitoshi, ni vizuri Waziri atueleze ni lini suala hili litatumika kisheria ili yeyote anayetumia mifuko hiyo ajue kuna faini ya kulipa au anaweza kufungwa jela. Bila sheria kuna baadhi ya watu wataendelea kutumia mifuko hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona kabisa mwaka huu mvua mfano kaskazini bado hazijanyesha lakini kwa kisingizio cha mabadiliko ya tabianchi, lakini ni wazi kuwa miti imekuwa ikikatwa ovyo kwa matumizi ya mkaa, wengine kwa ajili ya kilimo. Siku zilizopita vijijini (Serikali za Vijiji) ilikuwa ni lazima kupanda miti na ilikuwa hairuhusiwi kulima kando ya mito, lakini sasa hivi ni jambo la kawaida kufanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri shule zote za msingi na sekondari katika kila vijiji wawe na vitalu vya kupanda miti na iwe kabisa ni elimu kuanzia shule za awali kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira kwa kupanda miti na wajue ukikata mti lazima uwe umepanda mti mwingine. Wazee wetu walisomesha vijana wao kwa kukata mti na kuuza mbao lakini walihakikisha kuna mti mwingine pembeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nashauri kila halmashauri ziwe na vitalu vya miti ikiwezekana ya matunda pia ambayo yatatumika kujenga afya na kuongeza kipato kwa wananchi na uuzwe kwa bei nafuu ili kila mwananchi aweze kununua.