Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Susan Limbweni Kiwanga

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Mlimba

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa masikitiko makubwa sana hapa nilipo nalia. Silii kwa kupenda, nimetuma kwenye ma-group ya Wabunge, nimemtumia Waziri, kama kijiko kimezama barabara ya kutoka Ifakara - Mlimba hivi akina mama kutoka Mlimba wataendaje Hospitali ya Ifakara kwenda kujifungua?

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi kijiko kimezama (excavator) na yule mtoto anayesimamia pale kijiko kile alichokodisha cha baba yake amelazwa hospitali. Barabara hii imeshafanyiwa upembuzi yakinifu, imeisha mwaka 2017 lakini mpaka leo barabara hii haijengwi kwa kiwango cha lami. Chondechonde, hivi Watanzania wanaoishi Mlimba mnawahesabu wapo katika kundi gani nchi hii?

Mheshimiwa Naibu Spika, hali ni mbaya. Kama ni hali ya dharura basi iko Mlimba. Kila mkandarasi akipewa ile barabara kwa mwaka mzima aihudumie, akimaliza mkataba harudi tena kwa sababu ile barabara ni hatari, hivi tuseme nini mpaka muelewe? Ni dharura, naungaje mkono wakati barabara yangu haina lami? Naungaje mkono hii bajeti? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwa dharura, wataalam mnanisikia mko hapa. Ndugu Mfugale uko hapa, watu wa Mfuko wa Barabara mko hapa nendeni sasa hivi Mlimba mumpigie Eng. Makindi yuko Mlimba sasa hivi karibu wiki wanahangaika na barabara hii. Leo vyote mnavyojadili hapa mimi kwangu naona ni kizunguzungu, tunaomba barabara, imeisha upembuzi yakinifu mwaka 2017 kuna haja ya kujenga ile barabara ili kuokoa wananchi wanaotoka Mlimba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nachangia suala lingine kuhusu watu wa TAZARA. Leo nimepata taarifa ukaguzi wa ndani umebaini yule mhasibu na ameshasimamishwa bilioni moja point kadhaa zimeliwa. Watumishi wa TAZARA wanaostaafu sasa hivi wakienda kwa huyo mhasibu kudai mafao yao wanajibiwa mambo ya ajabu, lakini cha kushangaza Meneja wa Mkoa wa Tanzania ameongezewa muda wakati ameshindwa kusimamia mpaka mhasibu ametafuna hizo hela, sijui wanashirikiana? (Makofi)

Mheshimiwa Waziri, angalia suala la TAZARA. Serikali inalipa watumishi pesa kwa kodi za watanzania wengine lakini pale pale TAZARA kuna mchwa huyo anakula pesa. Nendeni mkaiangalie TAZARA. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na wastaafu nimeshapeleka faili kwa Mheshimiwa Kijaji, wale 1072 mpaka leo wengine wanakufa, mafao yao haijulikani, walistaafishwa kwa lazima wa umri wa miaka 55, mmewapunja, naomba muwape haki zao, tatizo nini? Leo nimeamua kulia na TAZARA na barabara ya Ifakara - Mlimba kilometa 126 point zake, mmeshafanya upembuzi yakinifu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawaomba kwa hali ya dharura hata tuma hapa mtaalam aende kule leo, hakuna gari inayopita, picha hizi hapa excavator limezama, gari gani itapita kwenye hiyo barabara ya TANROADS, hiyo ni dharura. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, watu watakufa kule wakina mama na watoto na wagonjwa watakufa kwa sababu tuna kituo cha afya kimoja tu Mlimba, basi madaktari wanne! Hospitali ya Wilaya ipo Ifakara, Hospitali ya Rufaa ya St. Francis ipo Ifakara, watu watafikaje huko?

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mpango, sawa mnaweka hela tu kwenye ndege, kwenye nini hatukatai tutaendeleza uchumi lakini wananchi wa Mlimba tuna shida kubwa, naomba mtupe barabara tuendelee na haya mambo mengine. Hizi ni kodi za Watanzania na wananchi wa Mlimba wanalipa kodi kama wanavyolipa wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba, simalizi hata dakika saba kwa uchungu, ninyi wenyewe mnajua nachangiaga mpaka kwa sababu nitamaliza vipi dakika saba, nataka majibu. Ningeomba Waziri aje na neno la dharura kuhusu barabara ya Ifakara mpaka Mlimba mnawaambiaje wananchi wa Mlimba. Asante sana. (Makofi)