Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara

Hon. Janeth Maurice Massaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe pongezi kwa Waziri na wasaidizi wote wa Wizara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, vikwazo ambavyo vinazuia maeneo yote EPZ kutoanzisha viwanda hapa nchini vitatuliwe. Mfano, eneo la EPZ Morogoro hatua za haraka zichukuliwe kwa kushirikisha Wizara ya Ardhi na TAMISEMI na kutoa maamuzi kwa haraka.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda vidogovidogo, SIDO ipewe uwezo mkubwa zaidi kwa kutengewa fedha za mafunzo kwa vitendo na kuwakopesha vijana mitambo midogo na ya kati na kuanzisha viwanda vidogovidogo kwa vijana kwa wilaya zote hapa nchini. Hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Dodoma uwekezwe kwa viwanda vingi vya mvinyo kutokana na zabibu ya Dodoma kukubalika katika soko la dunia.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwa100%.