Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara

Hon. Amb. Adadi Mohamed Rajabu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkono hoja na kuchangia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nawapongeza kwa kazi nzuri Mheshimiwa Waziri, Naibu Katibu Mkuu, Wakurugenzi na Watendaji wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumzie suala la shamba la mpira Muheza na Kiwanda cha General Tyre, Arusha. Napongeza kwa kuonekana kwa dalili za kupatikana kwa mwekezaji za kupatikana kwa mwekezaji wa kiwanda cha matairi. Nimefika na Kamati ya Bajeti na kuona kiwanda hicho, kwa kweli hakuna kiwanda pale, maana mwekezaji mwenyewe anapaswa kutoa mashine zote za zamani na atapaswa kuweka mashine nyingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kushauri kwamba kutokana na Muheza kuwa na shamba kubwa la mpira ambalo hapo awali lilikuwa linalisha kiwanda hicho bora, kiwanda hicho kijengwe kwenye maeneo hayo hayo ya shamba husika. Tutakuwa tayari kutoa eneo kubwa kwa ujenzi wa kiwanda hicho. Naomba wazo hili lipewe uzito wake au atafutwe mwekezaji mwingine atakayewekeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni kuhusu biashara. Hivi karibuni Kamati ya Bajeti ilikuwa Kampala, Uganda. Kule tulikuwa wafanyabiashara wengi wa Kariakoo na wengine wa nchi jirani, wakinunua vitu mbalimbali na kuvirudisha nchini au nchini mwao. Wafanyabiashara wote hao walikuwa na biashara zao Kariakoo na sasa wamehamia Kampala.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri kwamba Wizara ijaribu kuchunguza kuona ni jambo gani lililowafanya wafanyabiashara hao kuhama? Vile vile iangalie uwezekano wa kuwarudisha.