Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021

Hon. Charles Muhangwa Kitwanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia katika ajenda hii iliyoko mbele yetu. Tuanze kwanza kwa kutazama uchumi wetu na jinsi tulivyojipanga. Sisi sote tunatambua kwamba tuna vision 2025 na hii vision tukakubaliana kwamba tutai-cascade in five years plans. Plan ya pili tulionayo leo hii ni plan ya kuipeleka nchi yetu kwenye uchumi wa viwanda. Sasa tunafikaje pale kwenye uchumi wa viwanda Mheshimiwa Mpango pamoja na timu yake wameweka vizuri katika hotuba yao na katika maelezo ambayo tumeyapata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa sisi tunaitafsiri vipi na kuielewa na kuhakikisha kwamba ina-add value na kumwezesha kila Mtanzania aweze kusema kwamba yuko kwenye uchumi wa viwanda na anaishi maisha bora kuliko alivyokuwa zamani. Tuangalie kwanza nchi yetu imeajiri au watu wetu wanashughulika na kitu gani kwanza, asilimia kubwa. Tukiangalia tunakuta kwamba wananchi wengi wanashughulika na kilimo. Sasa viwanda vyetu vingi vielekezwe wapi na tutambue kwamba kuna viwanda angalau vya three categories; kuna viwanda vikubwa, mahitaji yake ni tofauti; kuna viwanda vya kati, mahitaji yake ni tofauti; na kuna viwanda vidogo ambavyo vitaweza kuajiri au kuwafanya wananchi wa kawaida washiriki wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vyote hivi vinahitaji mazingira yanayoeleweka. Nirudie tena nilishawahi kusema katika eneo letu la kwanza kabisa ambalo tuli-invest heavily lilikuwa ni eneo la madini, mwekezaji anapokuja kwenye madini anachukua madini anahama nayo, tukawapa incentives za kutosha wakaendelea wakawekeza kwenye madini. Sasa hivi tuko kwenye viwanda, viwanda hivi vinatakiwa vipewe incentives.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kitu kimoja tu. Mtu yeyote atakayekuja hapa atakuta ardhi, atakuta wananchi ambao watashiriki, atakuja na expertise na capital. Baada ya kujanavyo hivyo vitu, atajenga kiwanda. Sijawahi kuona hata mtu mmoja amejenga kiwanda akakibeba. Tuseme kwa mfano ametoka London, akakibeba akaendanacho London. Tuwape incentives hawa watu wajenge viwanda, hawatavibeba kutoka hapa kwendanavyo London. Madini tuliwapa incentives, wakabeba wakaendanayo leo tuna mashimo baadhi ya sehemu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisisitize sasa hili la kilimo. Kwanza naipongeza Serikali, inaweka miundombinu kwa ajili ya kupata umeme. Je, huu umeme mkubwa tunaoujenga kama hatuuwezeshi kuwa na viwanda vya ku-consume huu umeme, si tutaanza kuu-export huu umeme badala ya ku- add value ndani na kusababisha watu wakapata ajira; watakapopata ajira watalipa Pay As You Earn na zile pesa zitazunguka mifukoni mwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunapokuwa na kilimo, nichukulie mfano mzuri tu wa pamba; enzi ya Mwalimu pamba ilikuwa inanunuliwa na Vyama vya Ushirika na Vyama vya Ushirika vilikuwa heavily subsidized. Tulikuwa na viwanda (generies) vya kati na tulikuwa na viwanda vikubwa vya nguo. Vyote hivi vilikufa kwa nini? Hebu angalieni leo China; wengi tunavaa nguo kutoka China, wengi tunavaa nguo kutoka India. Policy yao kuhusu viwanda vya nguo ni nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huwezi kuwa na kiwanda cha nguo bila Serikali kuwa involved in one way or another. Kwanza kumbuka kwamba unahitaji a minimum ya kama dola milioni 50 ili uweze kununua raw materials ambayo ni pamba uweze ku-run mwaka mzima. Pamba ile utaihifadhi kwa mwaka mzima, kwa sababu, utakapokuwa unanunua pamba, ni msimu na sana sana ni miezi mitatu, baada ya miezi mitatu msimu umefungwa. Je, hiyo pamba utakayostahili kuwanayo kwa mwaka mzima, si lazima uwe na capital ya kutosha? Sasa kama una hela zako nyingi, na huwezi kuwa na cash money, itabidi ukakope. Kama unataka kukopa, hiyo interest rate ikoje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu tufikirie, leo hii kama kila Mtanzania anaevaa nguo kutoka China, asivae nguo kwa ku-save dola 10 tu, Watanzania wote, tuko milioni ngapi? Tuko milioni 55, lakini dola 10 tu kila mtu a-save anunue nguo ya hapa ili hiyo dola 10 izunguke kwenye uchumi wetu, tutakuwa tumezungusha hela kiasi gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hela hizo zitakapokuwa zimezunguka, si zitanunua vitu vingine ambavyo vimelipiwa ushuru? Ushuru huo utaupata kutokana na hiyo dola 10 kuwa imezunguka kwenye uchumi wako ukaweza kuuwezesha uchumi wako kukua. Kwa nini hawa watu wenye viwanda vya nguo wasipewe tax holiday au incentive kubwa hata ya ku-save dola 10 tu kwa kila nguo? Hilo ni jambo la kutazama. Tutazame: Je, watu wangapi watakuwa wameajiriwa kwenye viwanda vya nguo? Angalia MWATEX, MUTEX, KILTEX na kila mahali ambapo kulikuwa kuna viwanda kama hivi, vilikuwa vinaajiri watu wangapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka MWATEX wakati ule kilikuwa kinaajiri zaidi ya watu 1,000. Wacha hapo, wako wale wa kutengeneza zile nyuzi. Viwanda vile vya kati vya kuchambua pamba; kulikuwepo sijui Bukumbi, Buchosa, sijui wapi, kulikuwa na genery karibu 20; katika hiyo ilikuwa inaitwa Victoria Federation kwanza halafu ikawa Nyanza, ikaja SHIRECU na sehemu zote zile. Zote hizo leo hazipo. Maana yake wale wafanyakazi hawapo na kwa sababu hiyo sasa hakuna Pay As You Earn na kwa sababu wale wafanyakazi hawapo, hawana hela ambayo itawawezesha kusaidia kiwanda cha chumvi Uvinza kwa sababu wangeweza kununua chumvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuangalie ile trickledown na jinsi ambavyo tunaweza tuka-affect. Kwa hivyo, mipango yetu iangalie wapi tu-invest, wapi tutoe msamaha ili tuwezeshe viwanda vyetu na watu wetu waweze kupata faida kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nawaomba ndugu zangu, najua rafiki yangu Mheshimiwa Dkt. Mpango una akili sana na Naibu wako, hebu panueni zaidi tuione hivyo na muishawishi Serikali yote kwa pamoja, tuweze kuangalia ni kwa namna gani sasa tutatoka tulipo tuweze kweli kuwa nchi ya viwanda? Hatuwezi kuwa tunaimba tu bila kuangalia watu wengi ambao wanaguswa na eneo gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuangalie labda tena eneo la service au transport. Tunajenga SGR; very good plan na very long looking kama ambavyo Wajerumani walikuwa wanajenga reli kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza na kote walikuwa wanakwenda kuchukua raw materials. Sasa uchumi umebadilika, tunahitaji kujenga reli hii ili ituletee faida. Hatuwezi kujenga reli kwa ajili ya abiria wa kibinadamu tu, tujenge hii reli tukiwa na thinking kwamba, reli itakapofika Mwanza iweze kutusaidia kubeba mizigo yetu tuweze kui- export au tuweze kupeleka raw materials kwenye viwanda vidogovidogo ambavyo vimeajiri watu wengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna daraja zuri sana, natumaini litaanza kujengwa hivi karibuni pale Kigongo – Busisi. Very good decision again. Watu sasa hivi kwa sababu ya usafiri kutoka Kigongo kwenda Busisi, wakati mwingine malori yanajipanga kuanzia saa sita mchana linakuja linavuka saa sita usiku. Hayo ni masaa 12, lakini kama tutakuwa na lile daraja, litatumia dakika nne tu kutoka Kigongo kwenda Busisi na kuendelea na safari zake. Tutakuwa tume-save time na tutakuwa tumemwezesha huyo mtu kufanya business haraka zaidi. Sasa tu--add value kwa sababu vilevile pale Fela kutakuwa na dry port. Hatuwezi tu tukawa tunaleta mizigo inayotoka nje tukaiweka pale Fela halafu wananchi kutoka DRC, Burundi, Rwanda na Uganda wanachukua mizigo kutoka bandarini na kupitisha pale kwenye daraja. Lazima tuwe na mpango mkakati wa kujenga maeneo ya biashara kubwa, business centres.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikiwezekana pale kuwe na business centre kubwa, vifaa badala ya watu kwenda kununua Guanzhou watu walete au tuwashawishi wale wanye maviwanda kule Guanzhou walete pale Mwanza au eneo lolote karibu hapo. Sasa nguo au vifaa vyote vinavyoletwa pale vipewe tax free. Vikiwa tax free, Mtanzania unapokwenda kununua pale unalipia ushuru, unachukua vile vifaa vyako unaweza kuvitumia. Mtu anayetoka Rwanda, Kongo, Burundi nakadhalika akinunua pale, anapeleka Rwanda bila tax.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kikubwa ambacho mimi nakiona tuna shida kubwa ya uwoga na vilevile tuna shida kubwa ya kuona kama tutaibiwa. Tupige brain, tuweke control, tuweke system ambazo zitatuwezesha leo hii vifaa vinapokuwa hapa, unakuwa unaviona kwamba, huyu ameleta mizigo ya dola 1,000,000. Katika mizigo ya dola 1,000,000 labda 500,000 ameziuza localy, 500,000 amezi-re- export baada ya kuwa ame-import, lakini kwa sababu tuna wasiwasi inakuwa ni tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe mfano tu, tulikuwa na wasiwasi kweli kutumia hata hii. Tuliyapenda sana makaratasi, lakini leo hii you could see hapa kwenye meza zetu. Meza zetu ni safi, hazina matatizo and you will save a lot of money, tume-dare. Rais wetu ni very daring, let all of us be daring. Tu-dare kufanya, tukifanya makosa, tumwambie hapa nimekosea, nipe nafasi. Kama anaona hawezi kukupa nafasi, akutumbue, halafu tuendelee mbele, mwingine atakuja. Naye kama ni daring, mwishoni ataona hawa wamefanya hivi kwa nia njema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie tourism. Tourism again nimeiona hata humu kwamba tunanunua ndege tunaimarisha Air Tanzania, very good, briliant na matokeo yake tunayaona na trickledown again nimeshaizugumza. Ndege zetu sasa zinaruka kwenda Mumbai na Watanzania wanaleta mizigo, zinakuja na watalii, watalii wanakwenda kwenye mbuga. Watu kwenda kwenye mbuga hawaendi na ndege, wanaenda na Landrover ambazo zinaendeshwa na Watanzania. Wakifika Mlima Kilimanjaro kwa rafiki yangu Mheshimiwa Selasini, wale wanaozunguka ule mlima wanakuwa wapagazi, wame-gain wanapanda kwenda Mlima Kilimanjaro. Hiyo ndio trickledown ya uchumi na ndege zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tusiishie hapo. Wenzetu wa ATC wana mpango wa mpaka 2021, let us look beyond that. Tumeleta Dreamliner 8 mbili, let us think of having Dreamliner 9 mbili nyingine za market ya kwenda Israel na Ufaransa. Watu wengi wanaokuja hapa; sasa hivi ukiangalia, nilikuwa naangalia kwenye TV naona jinsi Waisrael wanavyokuja wengi na wanalalamika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri nina rafiki zangu wawili watatu kule, walikuwa naniambia, hivi nchi yenu inashindwaje kuwa na flight angalau mara tatu kwa wiki kuja Israel ili zitupunguzie gharama? Kwa sababu tunapokuja Tanzania, ndege tunazokujanazo tuna-charter mandege makubwa, it becomes very expensive kwa sababu anaenda mara moja, akirudisha, basi anaendelea kule, anaanza kutafuta market nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama tutakuwa na three times per week labda kutoka Tel Aviv na pale Israel kuja hapa, tutapata watalii wengi zaidi. Kwa hiyo, we should not be afraid, let us dare again to bring Dreamliner 9 mwaka 2023 mwaka 2024. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa biashara ya ndege, ndege hainunuliwi hivi hivi. You buy a slot; Unapo-buy a slot wanaweka kwenye kiwanda jinsi ndege zinazvyokwenda kama inafikia time yako ndiyo ndege inatoka. Kwenye kiwanda kama umeweka, wana-plan vizuri kwamba, itakapofika wakati wa kuweka engine, engine itakuwa imetolewa Rollsroyce imefika kwenye kiwanda inafungwa pale. Pale itakapofika, wewe ndio unahangaikahangaika, inafika wakati wa kuwekewa engine, engine hazipo, huwa hawasubiri. Inapita, engine itakwenda ifungwe huku pembeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo sababu ndugu zangu hapa wakati fulani wakati tunaleta ile Dreamliner 8 ya kwanza kwa sababu tuliinunua haraka haraka time ya kuiwekea engine ilikuwa imeshapita, slot yake ikawa imepita, engine zikafungwa nje watu wakaanza kusema aah, mmenunua ndege ambazo zina engine siyo za Rollsroyce, kumbe ile tumenunua slot ilikuwa ni too short, muda ukawa umepita wa kufunga zile engine zikafungwa badaye. Hivi, hamkuona aibu siku zinafika hapa na zina Rollsroyce? Hao ninaowasema wanajijua. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie umeme. Umeme tulionao sasa hivi we are looking at 2,150 Megawatt, very shortly, lakini kwa nchi kama ya kwetu kama kweli tutafuata mipango tuka-plan kama ninavyoshauri, huo hautatosha. Lazima tuwe na mixture. Maji yakikauka kama inatokea, siombei hilo, lazima tuwe na alternative. We should be thinking again kwenye mipango yetu ya viwanda hii, tuwe na umeme mwingine mkubwa wa level ya at least three thousand, five thousand Megawatt za makaa ya mawe. Leo hii tukianza kutengeneza, kufua vyuma hapa, umeme unaohitajika siyo huu mnaozungumzia. Kiwanda kimoja kinaweza kikahitaji 200 Megawatt na ndivyo hivyo viwanda vikubwa tunavyovizungumzia. Hapa mliokaa mbele, kaeni kwa pamoja, chakateni, tusitoe nafasi kwa watu ambao hawana environment nzuri kama sisi kupata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mfano mmoja, kuna kiwanda hapo nchi jirani sitaki kuitaja, nyuma yake kimeandikwa his excellence something her, halafu mwisho kuna e; wamejenga kiwanda na kilikuwa kijengwe hapa. Kinachoniuma zaidi, sasa hivi wanatengeneza magari ya kutumia umeme nchi hiyo na hao watu I brought them here. The bureaucracy we have in our system is so bad, mwishowe wakaenda Rwanda. Volkswagen sasa hivi zinatengenezwa Rwanda, ilikuwa kiwanda kijengwe hapa. Hebu tupunguze hiyo bureaucracy. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudie kwa kumalizia, anayejenga kiwanda hapa, hatakinyanyua kwendanacho. Hebu punguzeni hizo bureaucracy. Kama ataleta figisufigisu na kutaka kutuibia, hatakibeba, mwondoeni, wekeni watalaam wengine, Watanzania watakuwa wamejifunza, wataendeleza hicho kiwanda. It should not take six months ku-discuss issue ya kiwanda. Anaambiwa nenda hapa, nenda hapa, nenda hapa. Hivi kwa nini wenzetu wana-discuss mara moja mara mbili?

Mheshimiwa Mwenyekiti, I have so many bad experiencies ya kuleta wataalam au viwanda hapa halafu mambo yanakuwa hivyo hivyo, tubadilike. We should be business minded halafu wote tutumie coconut; wote humu ndani. Nilikuwa namsikiliza Waziri mmoja kwenye Baraza la Obasanjo, Mnaigeria, anazungumzia jinsi ambavyo tunasitasita na jinsi ambavyo hatuwezi kutoa maamuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumbukeni, dakika moja ikipita, ukitaka kuirudisha nenda kaburini. Utaikuta kaburini umeshakufa, kwa sababu ikishapita unasogea kaburini, ikishapita dakika nyingine unasogea na wote jinsi tunavyosherehekea mwaka mpya, yaani sherehe za kuzaliwa, kumbuka unasogea kaburini. Ahsante sana. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Kicheko/ Makofi)