Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Hon. Lucy Fidelis Owenya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kupata nafasi ya kuchangia.

Mheshimiwa Spika, Madaktari wa Mifugo. Kumekuwepo na upungufu mkubwa sana wa madaktari wa mifugo na kupelekea mifugo kufariki bila ugonjwa kutambulika na kueneza magonjwa hovyo. Pia kumekuwepo na kutopatikana kwa dawa za mifugo. Kwa mfano, unakuta kuna ugonjwa wa kichaa cha mbwa na chanjo hazipo na madaktari wa mifugo hawapo. Je, Serikali ina mikakati gani ya kuhakikisha madaktari wa mifugo na dawa zinapatikana? Siku za nyuma, madaktari walikuwa wanatembelea wafugaji na kutoa chanjo. Je, ni lini utaratibu huu utarudi?

Mheshimiwa Spika, sekta ya mifugo; wafugaji wengi wanajitahidi sana kufuga kisasa na kuzalisha maziwa mengi ambayo yangeweza hata kuuzwa nje, kutengeneza cheese, siagi na kupata nyama; lakini tatizo bado Serikali haijaweza kushirikiana kati ya Wizara na Wizara. Kwa mfano Wizara ya Mifugo kujenga viwanda vya maziwa ili kuweza kuwapatia wafugaji masoko. Je, nchi kama Tanzania kuna sababu ya kununua maziwa, siagi, cheese kutoka nchi za nje? Ardhi tunayo, mifugo tunayo, wafugaji wapo shida ni nini?

Mheshimiwa Spika, Ushauri; Serikali ijitahidi kila sehemu yenye wafugaji ihakikishe inajenga majosho ya kutosha ili wakati wa kiangazi mifugo isife kwa kiu; na ni vizuri kufanya hili katika kila Wilaya.