Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Madini

Hon. Ezekiel Magolyo Maige

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Msalala

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Madini

MHE. EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Spika, napongeza juhudi za Serikali kurekebisha sekta ya madini. Naunga mkono juhudi hizo na mipango ya Serikali kupitia bajeti hii.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali irekebishe na kusaidia wachimbaji kwenye maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, urasimu na mazingira ya rushwa katika utoaji wa leseni za uchimbaji; wachimbaji wadogo wa Msalala kupitia vikundi vyao vya KAGOMCO (Kasi Mpya Gold Mining Cooperative Society) na BMS (Bushimangila, Masabi na Segese Coperative Society) waliomba leseni maeneo ya Mwazimba na Bushimangila. Mheshimiwa Waziri Biteko alikuja Msalala na kuwahakikishia kuwa watapata leseni.

Mheshimiwa Spika, akiwa Bushamangila aliagiza hivyo, cha ajabu baada ya muda mfupi Afisa Madini Mkazi wa Kahama alihamishwa, afisa madini aliyeletwa alitoa leseni kwa mtu mwingine siku moja tu baada ya kufika Kahama, kinyume kabisa na maagizo ya Waziri; hiyo siyo rushwa? Naomba afisa huyo aliyetoa leseni Bushimangila kwa kampuni tofauti na BMS katika mazingira hayo ya rushwa achukuliwe hatua na leseni zitolewe kwa BMS.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa KAGOMCO waliomba leseni Mwagimba tangi 2008 na leseni yao kuingia kwenye mgogoro, naomba mno wapewe leseni yao kama Waziri, Mheshimiwa Biteko alivyoagiza.

Mheshimiwa Spika, kusiadia wachimbaji wadogo kupata exploration data za maeneo wanayofanyia kazi ili kupunguza hasara kwani maeneo mengi yalishafanyiwa exploration na GST na Sekta Binafsi na data hizo Serikali inazo au inaweza kuzipata.

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Msalala tunadai Acacia ushuru wa huduma miaka toka 2000 hadi 2014. Jumla ya madai ni dola 8,500, sawa na shilingi 16 bn. Naomba Wizara ya Madini kwa kushirikiana na TAMISEMI isaidie halmashauri yetu ilipwe haki yake.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.