Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

Hon. Janeth Maurice Massaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza sana Serikali kwa hatua kubwa ya mageuzi ya kiuchumi na kijamii ambayo yameushangaza ulimwengu kwa kipindi hiki cha miaka mitatu na nusu tu chini ya uongozi wa Awamu ya Tano. Pia, niwapongeze Waziri wa Fedha, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu na Watendaji wote wa Wizara ya Fedha na taasisi zake zote kwa kazi nzuri walizofanya kwa kipindi chote. Mwenyezi Mungu azidi kuwaongoza vema katika utendaji wao.

Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Tanzania kwa uzalendo mkubwa, upendo wake kwa Watanzania na nchi yake, kwa kuchukua hatua mbalimbali ambazo zinasaidia nchi yetu kusonga mbele kimaendeleo.

Mheshimiwa Rais wetu amekuwa jasiri, hodari na mbunifu mkubwa hasa kwa mambo ambayo yalishindikana kwa awamu zote za utawala wa nchi yetu. Ni Rais ambaye atakumbukwa na vizazi vya sasa na vizazi vijavyo, Mwenyezi Mungu azidi kumlinda na amjalie afya njema na neema tele.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na pongezi hizo, nina maoni/ushauri kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kilimo; Serikali ijenge maghala ya kisasa na vihenge vya kuhifadhia chakula ili kuzuia uharibifu wa mazao ya wakulima ambayo mengi yanaharibika kwa kukosa hifadhi.

Mheshimiwa Naibu Spika, masoko; kuwe na kitengo maalum cha kutafuta masoko nje ya nchi ya mazao mbalimbali na kipewe bajeti ya kutosha. Ukizingatia kuwa biashara ya mazao yetu ni lazima tuitangaze huko duniani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutenga maeneo makubwa ya kilimo; Serikali ichukue hatua ya makusudi ya kutenga maeneo makubwa ya kilimo na kuyatangaza ndani na nje ya nchi ili wawekezaji ambao wako tayari au wana nia ya kuwekeza kwenye kilimo, wachukue fursa hii. Watanzania pia washirikiane na wageni katika kuwekeza kwenye kilimo cha kisasa cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, mazao ya viungo; mazao kama karafuu, hiliki, pilipili manga, mdalasini, vanilla, mchaichai na viungo vingine. Mazao haya hayana utaratibu mzuri wa masoko, wakulima wa mazao haya wanahitaji mafunzo maalum ya jinsi ya kuendeleza kilimo chao na fursa ya mikopo kabla na baada ya mavuno ya mazao yao. Kwa mfano bei ya hiliki, karafuu, pilipili manga ni kati ya Sh.20,000 mpaka Sh.40,000, lakini walanguzi huenda kununua mti mmoja wa pilipili manga kwa Sh.50,000 ambapo mti mmoja hutoa kilogram 50. Hali hiyo inawanyonya wakulima wa viungo hapa nchini, tatizo ni kukosa huduma ya fedha kwa mazao ya muda mrefu, mazao haya yana soko kubwa nje ya nchi. Maeneo ya Morogoro, Muheza, Mbeya, Kigoma na kadhalika ndiyo kunakolimwa mazao hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.