Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi, Naibu Spika, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda sana nichangie katika Wizara hii hasa kwenye maeneo ya vyuo vikuu. Nataka niiambie Wizara ya Elimu kwamba, kumekuwa na vyuo vikuu ambavyo vinaendeshwa na taasisi za dini nchini Tanzania, lakini taasisi hizi tayari zimeanza kukata tamaa na kwamba, vyuo hivyo sasa hivi vinalegalega, havifanyi vizuri, lakini ninachofahamu ni kwamba, Wizara ya Elimu ndio walezi wa vyuo hivi. Kwa hiyo, ni vizuri sasa Wizara ikasimama katika kuhakikisha kwamba, hawa wanafanya vizuri kwa kuwasaidia resources mbalimbali ikiwemo pesa pamoja na watumishi ambao wanatakiwa wafanye kazi kwenye taasisi hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa hizi taasisi nazo pia zinafanya vizuri katika kuongeza elimu katika nchi yetu na zimekuwa zikifanya vizuri sana. Kwa hiyo, Wizara isimame katika eneo lake na kuhakikisha kwamba, wanawawezesha ili waweze kufanya vizuri zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa masikitiko makubwa sana imeonesha kwamba, vyuo hivi na taasisi hizi zinaendelea kufa hasa ninapozungumzia chuo kimoja pale Mkoa wa Mtwara. Nacho kimekufa, chuo hakifanyi vizuri na Wizara wapo, wamekaa wanaangalia tu. Pia kuna Chuo cha AJUCO, Songea Mjini, chuo kile kimekufa hakiendelezwi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimekuwa nikifikiria tu ni kwa nini Mheshimiwa Profesa Ndalichako anajisikiaje Nyanda za Juu Kusini kule vyuo vyetu vinakufa, yeye ni mama wa watoto yuko hapo na wala hatusaidii kuhakikisha kwamba, hawa wanaendelea kupata elimu na vyuo vile vinaendelea kufanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kipo Chuo cha St. Joseph Songea Mjini nacho pia hakifanyi kazi. Jana nilimtumia memo Mheshimiwa Profesa Ndalichako, nikasema naomba unieleze hivi vyuo vitafunguliwa lini? AJUCO ya Songea na Chuo cha St. Joseph cha Songea ni lini vitafunguliwa hivi vyuo? Maelezo aliyonipa kwa kweli, hayakuniridhisha na nasema Mheshimiwa Profesa Ndalichako leo hii wakati ana- wind up, naomba aje na majibu mazuri ya msingi ambayo yatani-stimulate niache kushika shilingi yake, vinginevyo nimpe taarifa kabisa kwamba, nakusudia kuzuia shilingi ya mshahara wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nataka niseme kwamba, hawa TCU wako kwa ajili ya kuhakikisha kwamba, vyuo hivi vinaendelea kufanya vizuri, lakini kazi wanayoifanya sasa ni kuzuia, kukataza vyuo visiendelee; hatuwezi kusaidia vyuo hivi viweze kufanya kazi endapo kama utaratibu utaendelea kuwa huu. Ni vizuri sasa Serikali isimame na TCU wafanye kazi yao ya kuwaelekeza na kuwasaidia, kuwashauri, ili vyuo hivi viweze kuendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kule kwetu Ruvuma kumekuwa doro, hakuna chuo chochote kile cha Serikali ambacho kitaweza kusaidia zaidi ya VETA, hakuna chuo kingine ambacho kitaweza kusaidia na uhitaji ni mkubwa sana. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Profesa Ndalichako awe makini na awe standby kabisa kwamba, nitazuia shilingi ya mshahara wako. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani sasa kijengwe chuo kikuu angalau kimoja katika Nyanda za Juu Kusini ambacho kitasaidia hasa katika Mkoa wa Ruvuma. Kijengwe chuo kimoja ambacho kitasaidia ambacho kiwe na program kama tatu hivi. Chuo kikuu hicho kwa sababu sisi katika Mkoa wa Ruvuma tunalima mazao mchanganyiko sana, kwa hiyo, nadhani kwamba, kuwe na program tatu katika chuo hicho kitakachoanzishwa ambazo ni crop program. Crop program itasaidia kuendeleza shughuli za uzalishaji kwenye sekta ya kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nyingine ni Chemical Engineering. Sisi tunalima kule korosho na kahawa, tulidhani sasa hii chemical engineering itasaidia hii program kuhakikisha kwamba, eneo lile linaendelea kustawi kupitia hizo program. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tuna Ziwa Nyasa. Ziwa hili limetulia tu halina mwendelezo wowote. Kwa hiyo, nadhani kwamba, kukiwa na program ya fisheries itasaidia sana kuwainua vijana wetu na watafanya uwekezaji kwenye ziwa ambalo linaonekana. Mheshimiwa Profesa Ndalichako ni mtani wangu, lakini leo mimi sina utani naye. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesisitiza sana kwamba, Wizara isaidie hivi vyuo. Nakumbuka Awamu ya Tatu ya Mheshimiwa Benjamin William Mkapa ilisaidia chuo ambacho ni University of Morogoro, University of Morogoro walisaidiwa wao walikuwa na shida ya majengo, lakini Mheshimiwa Rais aliweza kutoa maelekezo wakapewa majengo ya TANESCO na yale majengo yaliwasaidia. Sasa ni kwa nini Mheshimiwa Profesa Ndalichako hasaidii vyuo vya Songea vile vilivyofungwa ili viweze kufunguliwa? Ana ajenda gani wakati Kusini sisi kule hatuna chuo chochote? Tunamwomba tafadhali sana, yaani kule Mkoa wetu umepooza, hakuna vijana wanaoendelea katika shughuli za kusoma kupitia vyuo vikuu. Nakuomba sana, tafadhali sana, nilitaka kulia ila kwa sababu ni Mwezi Mtukufu, kwa hiyo nimeacha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ni kwanini Mheshimiwa Ndalichako husaidii vyuo vya Songea vile vilivyofungwa ili viweze kufunguliwa? una agenda gani wakati kusini sisi kule hatuna chuo chochote tunakuomba tafadhali sana yaani kule Mkoa wetu umekuwa umepooza hakuna vijana wanaoendelea katika shughuli za kusoma kupitia vyuo vikuu. Ninakuomba sana tafadhali sana nilitaka kulia ila kwasababu Mwezi Mtukufu kwa hiyo nimeacha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Prof. Ndalichako naomba wasaidiwe hawa vyuo hivi vya taasisi za dini waweze kama kuna shinda ya majengo wapewe majengo lakini kama kuna shida ya fedha wapewe fedha, lakini pia kama kuna masuala ambayo yanahusiana na masuala la management nayo pia nimeambiwa kwamba ili chuo kiendelee lazima kuwe na ma-professors ina maana Mheshimiwa Prof. Ndalichako wewe ulikuwa Mwalimu wa vyuo vikuu huna ma-professors utupelekee kule vyuo vile vifunguliwe.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa.

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naunga mkono hoja nakusudia kushika shilingi ya Mheshimiwa Prof. Ndalichako. (Makofi)