Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo

Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

3

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii nichangie katika Wizara hii nyeti ya Kilimo. Labda niombe tu kusema kwamba nilisikia vizuri au nilijisikia vizuri nilivyoona Waziri akisema kwamba hiki kilimo ambacho kinaendeshwa na asilimia 65 ya Watanzania hakina tija. Kwa mantiki hiyo nika-expect kwamba atakuja na mpango mkakati wa kwamba tuwe na commercial farming ya big farmers ambao wataweza ku-supplement kulima kilimo hiki cha wenzetu hao wadogo.

Mheshimiwa Spika, mwisho nikajiuliza kwamba kwakweli sijaweza kuona kama tunasheria ya kulinda ardhi ya kilimo najua tunasheria ya kulinda mazao kahawa, tumbaku lakini sijui kama tuna sheria ambayo inalinda ardhi ya kilimo. Kwanini ninasema hivyo unakuta mara nyingi kumekuwa na hii migogoro ya kuingiliana Wafugaji na Wakulima moja, lakini la pili Serikali ikitaka kujenga mahali inakwenda kufukuza wakulima wanasema tunataka nafasi hii tugeuze tuwe tunajenga aidha Ofisi za Serikali au tujenge shule kiasi kwamba mkulima anajiona kama mtumwa katika nchi yake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wewe umeji-establish kwa miaka mingi ile sehemu umeitafuta ukajua kuna maji pake lakini sasa inakuja Serikali inasema itaku-compensate hakuna kukaa ku- negotiate hakuna kuna kwamba unanihamisha unanipeleka wapi? Haiwatafutii hata mahali pa kusema ndio wana settle kwa ajili ya kujenga nyumba zao na kulima. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, matokeo yake mashamba ambayo mkulima ameyaboresha kwa muda mrefu anapewa fedha kidogo anaambiwa nenda utatafute sehemu nyingine, swali ni kwamba kule anakoenda kutafuta ana uhakika gani baada ya miaka mitano hatahamishwa tena kwa hiyo, nilikuwa ninaomba nipate hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini lingine sisi najua Tanzania hatuna uzoefu wa kulima kilimo cha umwagiliaji in such commercially sasa ninajiuliza hivi kwanini hatuendi kujifunza kwa wenzetu Kenya, kwanini hatuendi kujifunza kwa wenzetu South Africa! Kwamba ardhi lazima utenge ardhi kubwa kuonesha kwamba hizi hekta labda 100,000 au hekta 200,000 tuna-specialize kwenye mazao say Alizeti. With that tunakuwa forward na backward linkages ambapo utaweza kuweka miundombinu inayotakiwa, miundombinu ya umwagiliaji, miundombinu ya umeme na barabara hapo hapo unaweka kiwanda kitakacho-process tuna vijana wetu wanamaliza SUA tuna vijana wetu wanamaliza vyuo vingi hivi vya Kilimo, hawana ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini suppose Serikali ingekuwa imetenga haya maeneo makubwa na hati zipo wakatengeneza infrastructure wakawasaidia hawa vijana wakawapa mikopo ya kama miaka mitano bila kurudisha ili waweze ku-produce hiyo si inge-create ajira ambayo ingehakikisha vijana wetu wanashiriki katika uchumi wa nchi hii.

Mheshimiwa Spika, najua kwamba kuna-documents in come across imeandikwa na Mmarekani mmoja wanasema ‘American needs to keep Africa impoverished ili nchi za Marekani, Ulaya, Asia waendelee ku-survivor. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo sasa hivi kilimo chetu kinategemea fedha za umwagiliaji kutoka kwa donners na hivi fedha kwa 90 percent hizi fedha haziji intime.

Mheshimiwa Spika, maana yake zitukwamishe ili tushindwe tuendelee kuwa impoverished kwa hiyo, ningeomba kwamba kama Serikali ipo serious itenge fedha za umwagiliaji nakumbuka mwaka 2019 kulinunuliwa mitambo ya kuchimba mabwawa Mheshimiwa Bashe labda anaweza kukumbuka lakini sijui kama ile mitambo mpaka leo imetumika na kama imetumika imetumika wapi? Kwa hiyo, ina maana nchi yetu tunaweza kuweka mikakati mizuri lakini utekelezaji ukawa mbaya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukiangalia nchi zetu za Kiafrika, Afrika nzima ni kubwa inafikia ukubwa ukiunganisha Marekani, China pamoja na Europe lakini leo tunakwenda China kuomba misaada kwa nini, lazima tujiulize kwamba mipango yetu tunayoipanga siyo mizuri na kama Kilimo ndio tunategemea kitutoe basi lazima kipate priority na kiwe well planned ili tujue kwamba kweli tunaweza kutoka katika umaskini huu. Kwa hiyo, ninachoona ni kwamba Wizara zetu hazina mawasiliano. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)