Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maliasili na Utalii

MHES. RASHID SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi hii. Naomba nichukue nafasi hii kuipongeza sana Wizara, Mheshimiwa Waziri, pamoja na Mheshimiwa Naibu Waziri wanafanya kazi nzuri sana ambayo imeanzia kwenye kule ku-plan jezi ya wekundu wa Msimbazi kwa kuweka lile jina la Visit to Tanzania, naamini kabisa kwamba tutaona athari chanya za neno lile muda si mrefu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa kushauri mambo kadhaa katika Wizara hii. Jambo la kwanza nataka niwaarifu Wizara kwamba, Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi inapakana na wilaya nne; Wilaya ya Mwanga, Same kwa Mkoa wa Kilimanjaro, lakini kwa Mkoa wa Tanga, kuna Wilaya ya Lushoto pamoja na Wilaya ya Mkinga. Sasa mara zote Mawaziri wanapofanya ziara wanakwenda Mkoa wa Kilimanjaro pekee. Sasa nataka niwaambie na Tanga ipo kwa maana ya Lushoto na Mkinga, inapatikana Hifadhi ya Taifa Mkomazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kule tuna changamoto ya tembo wamevamia katika miji kadhaa hasa katika Tarafa ya Umba, Kata ya Mnazi na Kata ya Lunguza, Vijiji vya Mkundi Mbaru na Mkundi Mtae kule tembo wanasumbua sana. Juzi wamemwona Naibu Waziri yuko Kilimanjaro wakasema huyu Mheshimiwa Naibu Waziri mpaka asikie tumevuna tembo ndiyo afike hapa. Kwa hiyo namwomba sana afike eneo lile akatatuwe matatizo ya wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine nataka nichangie kuhusu soko la utalii. Wizara hii kuna maeneo ambayo inakosea, tunasubiri watalii waje wenyewe Tanzania kwa kutumia tour operators wa Kitanzania. Nataka niwaambie kwenda kwa stahili hiyo ya kuvua samaki walioko kwenye kapu haitatusaidia, ni lazima tujitahidi twende kule ambako wanapotoka. Kuna festival kubwa mbili zaidi duniani; ya kwanza iko kule South Africa ambayo wanaita Indaba, iko kama ile Karibu Festival ya Arusha, lakini hii ya South Africa inakusanya Mataifa ya Afrika, Ulaya pamoja na Mataifa ya Amerika ya Kusini. Hali kadhalika kule Ujerumani Berlin, nako kuna shoo kubwa sana ya mambo ya utalii. Kule ndiko Wizara inapaswa kwenda kukutana na tour operators wa kimataifa wale ndio wanaosukuma watalii kuja katika nchi zetu, lakini tutakapokuwa tunasubiri huku itakuwa sio kazi rahisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tumwombe sana Mheshimiwa Waziri sana, yeye ni Mngoni na ame-migrate kutoka South Africa, sasa asikae Wizarani,atoke aende huko duniani akatuletee watalii.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine nataka kuchangia kwenye eneo la vitalu vya uwindaji. Uwindaji ni sekta ambayo imefifia. Mwaka 2013 tulipata wawindaji takribani elfu 1,550, lakini mwaka 2018 kabla hata ya covid walishuka mpaka 473. Kuna mambo fulani tuliyafanya pale ambayo tulikosea, ikiwa ni pamoja na kuongeza ile tozo ya leseni ya vitalu kutoka dola 30,000 kwenda dola 85,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo niombe sana sisi nchi yetu jiografia imetawanyika sana, mwindaji anapotoka Ulaya, anakuja aidha Kilimanjaro International Airport, Dar es Salaam ama Zanzibar, anahitaji tena kuchukua charter flight kwenda Selous, kwenda Katavi, kwenda Burigi wakati huo kabla haijawa hifadhi kwa ajili ya kufanya huu uwindaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kuna gharama nyingine ambazo wanazipata. Hivyo, sasa tutengeneze inclusion ya kupunguza gharama hizi ili tuweze ku-facilitate hizi shughuli za uwindani katika maeneo ambayo yako scattered.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Sekta nzima ya Utalii nataka niwaambie, tuna advantage kwa mwaka huu kwa sababu hata Zanzibar watalii waliopatikana mwaka uliopita na mwaka huu ni wengi zaidi kuliko historia ya utalii Zanzibar. Hii ni kwa sababu covid kote duniani wanajua Tanzania ndio sehemu ambayo ni covid free, kwa hiyo wenzetu Wazanzibari kwenye eneo la utalii watakuwa mashahidi, miaka hii miwili wamepokea watalii wengi sana.

Kwa hiyo na sisi tuboreshe tu mazingira tuangalie tozo zetu zimekaaje tuweze kupata hiyo advantage ya kuwa covid free kwa ajili ya kuvutia watalii wengi sana kuja kutalii katika nchi yetu. Otherwise nawapongeza wanafanya kazi nzuri, waendelee hivyo hivyo. Namshukuru pia hata akienda pale uwanja wa Taifa yeye kama yeye magoli huwa yanakuwa mengi zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)