Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

Hon. Abdi Hija Mkasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Micheweni

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

MHE. ABDI HIJA MKASHA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na uzima na nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa mahiri katika majukumu yake ya kila siku namuombea kwa Mwenyezi Mungu uhai na uzima katika maisha yake yote na pia nampongeza Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha kwa uwasilishaji wake wa bajeti iliyosheheni Tanzania kwa ujumla.

Mimi napenda kuchangia moja kwa moja kwenye sehemu mbili kama ifuatavyo; mosi napenda kuchangia katika Wizara ya Uvuvi na Mifugo kwa kuwa nchi yetu Mwenyezi Mungu ameibarikia rasilimali ya bahari na maziwa. Mimi naishauri Serikali yangu kuitumia vyema rasilimali hizi tulizonazo kwa kuwanyanyua wavuvi wetu wadogo wadogo ili waweze kujikimu kwa pamoja na kulipatia faida Taifa letu kiujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili ni suala zima la Jeshi letu la Polisi; kiukweli Jeshi letu la Polisi linafanya kazi kubwa mno katika Taifa letu, lakini ni vema Serikali itazame upya suala zima katika stahiki zao kwa vile kipato chao si kikubwa, ni vema waangaliwe upya lli waweze kuonekana na wao. Kwa bahati mbaya huwa wanapatiwa refreshers course kwa ajili ya kuwapa utayari wa majukumu yao ya kila siku, lakini huwa wanajigharamia wenyewe. Jambo hili linawapa askari wetu wakati mgumu na hawatokuwa na morali na kama huna morali katika kazi za kila siku hata ufanisi wa majukumu ni lazima yatakuwa madogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naishauri Serikali ilione na hili ili waweze kuwa na morali ili waweze kufanya vyema kazi zao zaidi, lakini pia na Idara yetu ya Uhamiaji ikumbuke kwamba Tanzania Zanzibar kiujumla ni nchi ambayo ni Visiwa. Visiwa vile vimezungukwa na bahari, sasa huwa kuna bandari bubu nyingi sana. Naishauri Serikali ni vyema inunue boti za kisasa ambazo kwa kushirikiana na Uhamiaji na Jeshi la Polisi ili waweze kufanyia doria katika maeneo yetu yaliyotuzunguka kwa lengo zima la kuwasaka wale wafanyabiashara haramu pamoja na wahamiaji haramu ili kudhibitiwa wakati wanapokuwa katika kazi zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha na naunga mkono hoja.