Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Hon. Sadifa Juma Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Donge

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

MHE. SADIFA JUMA KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipatia nafasi. Kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza leo nichukue nafasi hii kuwashukuru sana wananchi wangu wa Jimbo la Donge kwa kunichagua tena kuwa Mbunge kwa kipindi cha pili sasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue nafasi hii kulipongeza sana Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Nawapongeza kwa kazi nzuri, mwanana na yenye kuvutia wanayoifanya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwaambie rafiki zangu sitawatukana, wewe nisikilize tu na ndiyo maana nimekaa ukanda wa Gaza makusudi. Nataka niwaambie marafiki zangu, mshukuruni sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Washukuruni sana hawa watu wafuatao, Waziri wa Ulinzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi, Mheshimiwa Dkt. Shein, Mkuu wa Majeshi hawa watu ni wastaarabu sana, waungwana sana, washukuruni sana hawa watu. Kwa nini nasema hivyo?
MHE. SADIFA JUMA KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli usiopingika mwenye mamlaka ya kutangaza matokeo ni Tume ya Uchaguzi, ndiyo utaratibu tuliojiwekea. Leo anajitokeza mhuni mmoja anajitangaza yeye ndiyo Rais, hebu niambieni nyie, nchi gani, jeshi ganiā€¦
MHE. SADIFA JUMA KHAMIS: Kama kuna mtu anaweza kuja kunipiga aje mimi nasema. Nchi gani, jeshi gani ambalo mtu amejitangaza kuwa Rais halafu limuachie tu kienyeji hivi hivi? (Makofi/Kicheko)
MHE. SADIFA JUMA KHAMIS: Nawaambia washukuruni sana, hawa watu hawa wamewasaidia, wapongezeni.
TAARIFA
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sadifa naomba ukae ili upewe taarifa...
MHE. SADIFA JUMA KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli usiopingika, vyombo vya habari vipo, Maalim Seif Sharif Hamad alijitangaza kuwa Rais wa Zanzibar kwamba yeye ndiye aliyeshinda, alijitangaza mwenyewe.
MHE. SADIFA JUMA KHAMIS: Ndiyo maana nasema kwa kupitia kitendo hicho ni uhuni na hii kauli siifuti, ni uhuni.
MHE. SADIFA JUMA KHAMIS: Nawaambia mshukuruni sana Dkt. Mwinyi, Waziri wa Ulinzi angekuwa Sadifa nawaambia mngekuwa mnavuja nyie! Msiniulize wapi panapovuja, nawaambia kweli! Kwa nini niwaambie uwongo huo ndiyo ukweli.
MHE. SADIFA JUMA KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika, mwenye mamlaka ya kuteua wakuu wa mikoa ni Rais pekee wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Bara lakini kwa upande wa Zanzibar ni Rais wa Zanzibar.
(Hapa baadhi ya Waheshimiwa Wabunge walikuwa wakiongea bila mpangilio)
MHE. SADIFA JUMA KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwaambie wenzangu hawa, wote aliowateua Rais siyo Wanajeshi wale wameshastaafu.
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sadifa naomba ukae.
MHE. SADIFA JUMA KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika...
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sadifa naomba ukae. Mheshimiwa Malembeka mchangiaje wetu wa mwisho.