Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017

Hon. Juma Hamad Omar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ole

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017

MHE. JUMA HAMAD OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nataka kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunipa fursa hii adhimu ya kuchangia taarifa hii muhimu, taarifa ya Kamati ya Bajeti, katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Januari, 2016 hadi Januari, 2017.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Bajeti, nadhani Mheshimiwa Mwambe amezungumza mengi sana na taarifa yenyewe ina mambo mengi sana na muhimu, sasa mimi nitachukua nafasi hii kukazia tu baadhi ya sehemu ambazo nadhani zina umuhimu wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yoyote duniani inapata sifa sana ya maendeleo ya kiuchumi ikiwa itakuwa na mambo matatu yafuatayo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kwanza nchi hiyo inatakiwa iwe na sera sahihi ya uchumi (Prudent Economic Policy); pili, nchi hiyo iwe na sera sahihi ya utozaji kodi (Taxation Policy); tatu, iwe na sera sahihi ya fedha (Prudent Fiscal and Monetary Policy). Sasa mambo hayo matatu yapo katika kapu ambalo linaitwa good governance and political stability. Maana hata hayo mambo matatu kama unayo, lakini kama huna good governance na political stability basi huwezi kuendelea kiuchumi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani mtakubaliana na mimi kwamba ziko nchi nyingi sana duniani, ambazo zimepiga sana hatua za kiuchumi. Kwa mfano, tuchukulie nchi za mashariki ya mbali (far east) nchi zile zimepiga sana hatua. Tukichukua kwa mfano utawala wa Mahathir Mohamad katika nchi ya Malaysia; Mahathir Mohamad alikuwa ni Fourth Prime Minister wa Malaysia, na nina hakika mtakubaliana na mimi kwamba kama kuna mtu alihuisha uchumi wa Malaysia au kama kuna mtu aliujenga uchumi wa Malaysia wa kuja na prudent economic policies, prudent of fiscal and monetary policy, prudent taxation policy basi alikuwa ni Mahathir Mohamad. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Malaysia ya leo ni nchi moja ambayo imepiga a very big economic strive, hivyo nchi nyingine za mbali ya Mashariki. Tuje hapa kwetu Afrika, Botswana ni nchi ambayo ina-enjoy the highest per capital development. Nchi ile haina resource nyingi kuliko Tanzania, nadhani kama sikosei resources zao zaidi wanazotegemea ni madini kidogo na mifugo, lakini leo Botswana ina the highest per capital income, lakini kwa nini? Botswana imefikia pale kwa sababu ya good governance and stability. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani hata ukichukua ile award ambayo ametoa Mo Ibrahim award ile imetolewa kwa Marais wastaafu ambao wamekuwa na a very good governance and good political stability. Rais wa Botswana mwaka 2008, Mheshimiwa Festus Mogae alipata zawadi ile ya dola 5000. Rais Kikwete amestaafu juzi nadhani atapata, lakini sasa kama hii imemaliza 2016 hajapata unaanza kujiuliza ni kwa nini? Kwa hiyo, good governance ni kitu muhimu sana katika yote haya. Botswana ukichukua kigezo cha uchumi cha foreign exchange value, Botswana ina foreign exchange ya kutosha kwa miezi 12. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Nigeria pamoja na kwamba ni old producing country lakini ana foreign exchange ya kutosha kwa miezi kumi kwa sababu kule ndani kumekuwa na political terms, tukija kwetu Tanzania tuna foreign exchange ya kutosha kwa miezi minne, tukija Zimbabwe rafiki yetu ambaye tunampenda sana na tunashirikiana naye sana because of lack of good governance ana foreign exchange siku saba this is amazing! Kwa hiyo, yote mifano inamaanisha kwamba haya mambo matatu, lazima yawe katika kapu la good governance, without good governance you can not make strong economic strives. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuje kwenye Pato la Taifa na tunaambiwa linaongezeka, mwaka 2016/2017 Pato la Taifa tulitegemea kwamba litakuwa asilimia saba lakini tukienda mwaka 2017/2018 itakuwa asilimia 7.2. Swali la kujiuliza infact katika hii region yetu sisi ndiyo tunaongoza kwa Pato la Taifa wanafuatia Rwanda, wanafuatia Kenya. Rwanda katika mwaka 2015 walikuwa na Pato la Taifa la asilimia 6.9; mwaka 2016 matarajio ni kwamba watakuwa na asilimia sita. Kenya ni ya tatu lakini nchi nyingine hizi kama Burundi, Uganda, Zambia, Malawi, Congo DRC zote tunazipita sana.
Kwa hiyo, the first economy in our region ni Tanzania, ni asilimia Saba lakini tunategemea kupata asilimia 7.2. Swali la kujiuliza kama Pato la Taifa linaongezeka kiasi hicho hivi kwa nini hali za wananchi wetu zimekuwa duni? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nasema nikingalia tu, ni kwa sababu sekta inayo-employ watu wengi katika Tanzania ni sekta ya kilimo; na Government yetu haijafanya a big investment katika sekta ya kilimo. Sekta ya kilimo inachangia only 2.1 percent ya Pato la Taifa, sekta ya mawasiliano nadhani kama sikosei inachangia asilimia 15.5, sekta ya uchimbaji madini ndiyo kubwa inachangia asilimi 15.8, lakini sekta ya uchimbaji madini inaajiri watu wa nje. Sekta ya mawasiliano na uchukuzi sawa lakini haina direct impact na mkulima, lakini kwa sababu Serikali haija-mark very big investment over areas katika sekta ya kilimo ndiyo ukakuta leo sekta ya kilimo ambayo imaajiri watu wengi, inachangia only 2.1 percent. Hapa inaonesha kwamba hatuna a prudent economic policies kupanga ni kuchagua. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija hapo hapo kwenye Pato la Taifa, mimi nakubali fine Tanzania is a fast growing economics in terms of GDP, lakini that is a nominal terms. In real terms tunakwenda chini; wakati tunazungumza Pato la Taifa linaongezeka lakini pato la kila Mtanzania linapungua in real term. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2014 kwa mfano pato la Mtanzania kwa wastani alikuwa anapata dola 1,047, lakini mwaka 2015 imeshuka anapata dola 966.
MBUNGE FULANI: Mhh!
MHE. JUMA HAMAD OMAR: Ndiyo! Hii ni kwa sababu sekta ya kilimo ambayo kwa kweli ilikuwa tuweke priority na ambayo inaajiri watu wengi but government has done nothing when it comes to investment.
Sasa kama hatuja-invest kwenye sekta ya kilimo ambayo inaajiri watu wengi nakuhakikishieni in real term fine, wataalam wanatuambia Pato la Taifa linaongezeka but in nominal terms pato haliongezeki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja kwenye mapato (taxation policy); hakuna Serikali yeyote duniani ambayo inaongozwa….
MWENYEKITI: Tunaendelea!