Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Hon. Magdalena Hamis Sakaya

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Kaliua

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Spika, pongezi kwa Mheshimiwa Waziri, Naibu wake na watendaji wote kwa kazi na kuandaa hotuba hii.

Mheshimiwa Spika, nchi yetu na Serikali tumekuwa na kasumba ya kutokuwekeza kikamilifu fedha ya kutosha kwenye michezo na hilo suala la kuwezesha michezo mbalimbali kuachwa kwa wahisani, mashabiki na wapenda michezo.

Mheshimiwa Spika, tumekuwa tunashuhudia tunapeleka team kambini kwa maandalizi ya mashindano ya Kimataifa lakini wachezaji wanalalamika hata chakula wakiwa kambini hawapewi inavyostahili, hii ni aibu kwa Taifa huwezi kuvuna bila kupanda.

Mheshimiwa Spika, miaka ya nyuma michezo mashuleni ilipewa uzito na kipaumbele kwa maana tangu primary school tulijengewa misingi mizuri ya kuifahamu vizuri mchezo, lakini pia kusaidia wanafunzi kwa sasa shule nyingi hasa shule za umma hakuna jitihada zozote za kuendeleza michezo na hakuna walimu wa michezo.

Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha tunajenga vipaji vya watoto bado mapema, Serikali ieleze Bunge mikakati ya kuhakikisha kwenye mashule yote kuna Walimu wa michezo wenye ujuzi wa michezo. Serikali ieleze mikakati ya kupeleka vifaa vya michezo kwenye shule za umma ili watoto wapate fursa ya kushiriki michezo na kujenga afya na akili zao.

Mheshimiwa Spika, viwanja vingi vilivyotengwa kwa michezo maeneo mbalimbali vimevamiwa na kujengewa makazi na Serikali inalijua hili, Serikali ieleze Bunge viwanja vyote vya michezo nchini vinalindwaje, visivamiwe lakini pia ni mikakati gani ya Serikali kurejesha viwanja vilivyovamiwa.

Mheshimiwa Spika, tumekuwa tunashuhudia watoto wakitumika kwenye michezo ya maigizo na hivyo kuwapotezea ndoto zao lakini pia kuwajengea taswira hasi kwa michezo inayotisha. Serikali itoe maelezo ya kutosheleza ni kwa nini watoto wanatumika kwenye maigizo?

Mheshimiwa Spika, katika Taifa letu maeneo mengi ya pembezoni mwa nchi, usikivu wa redio ni hafifu sana na maeneo mengine hakuna kabisa, mawasiliano ya redio. Je, kuna mpango gani wa Serikali kuhakikisha mawasiliano ya redio yanafika pande zote za Taifa hili ili kila Mtanzania apate haki ya kusikia na kujua yanayojiri ndani ya nchi yake.

Mheshimiwa Spika, katika Jimbo langu la Kaliua yapo maeneo ya Kata nyingi ambayo usikivu ni hafifu sana na pengine hakuna kabisa. Kata hizo ni Kata ya Igwisi-Kijiji cha Igwisi, Kijiji cha Mpanda mlohoka; Kata ya Usimba-Vijiji vya Usimba; Kata ya Ushokola-Kijiji cha Ukikubi; Kata ya Zugimlole- Vijiji vya Igombe na Luyombe; Kata ya Ukumbi Siganga-Vijiji vya Usinga na Ukumbi kakonko; Kata ya Usingi, Kijiji cha Kombo na Luganjo; Kata ya Usonye, Vijiji vya Luganjo, Mtoni, Shela na Maboha; na Kata ya Uganga-Vijiji vya Mkuyuni, mpilipili na limbula. Serikali ieleze kuna mipango gani mahsusi kuhakikisha mawasiliano na usikivu katika maeneo haya unapatikana.

Mheshimiwa Spika, miaka ya nyuma mchakato wa kumpata Miss Tanzania ulikuwa unavutia na waliochaguliwa walituwakilisha vizuri Kimataifa. Kwa kuwa kwa sasa suala hili limepoteza mvuto na kuendeshwa kwa rushwa kubwa na udhalilishaji. Serikali ifute uwepo wa zoezi hili kwa heshima ya Taifa.