Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia kwa maandishi hotuba hii ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Pili, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kuandika kwa ufanisi hotuba ya Wizara yao. Nawaombea kila la kheri katika majukumu yao.

Mheshimiwa Spika, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC); Shirika la habari ni chombo muhimu katika nchi kwa kuelimisha na kupasha habari wananchi wake. Bado kuna matatizo makubwa kwa wananchi wa vijijini ya usikivu usioridhisha. Wananchi wanashindwa kupata matokeo muhimu ambayo ni haki yao. Ushauri wangu katika hili ni kwamba, Serikali kuboresha miundombinu ya TBC kwa kununua vifaa vya kisasa vitakavyoondoa kabisa tatizo hili. Aidha, Serikali iongeze kasi ya kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa Shirika hili.

Mheshimiwa Spika, Sekta ya maendeleo ya michezo; michezo ni jambo lenye manufaa makubwa katika nchi. Michezo inajenga afya pia inaleta uhusiano mwema kati ya Mataifa duniani. Taifa letu limekuwa likidorora sana kwenye sekta ya michezo yote hasa ya mpira wa miguu, hii ni kutokana na matayarisho mabovu katika kuwapata wachezaji wa mpira. Ushauri wangu katika hili ni kuwa, ni vyema Serikali ikaweka sera maalum na endelevu ya kuwapata wachezaji. Ni vyema kuwa na timu ya kudumu ya na siyo kuendelea na utaratibu wa sasa ambao wachezaji hukusanywa pale tu wanapohitajika na kuruhusiwa kuondoka baada ya kumaliza mchezo husika, hali hii siyo ya tija hata kidogo.

Mheshimiwa Spika, ushauri wa pili katika kuwapata wachezaji walio bora ni Serikali ingekuwa na utaratibu maalum wa kuweka somo la michezo katika shule maalum ya michezo. Hii ingerahisisha kuwapata wachezaji wenye viwango ambao watakuwa wameandaliwa kuanzia udogoni (watoto wenye umri mdogo).

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.