Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Tundu Antiphas Mughwai Lissu

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Singida Mashariki

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kunipa fursa ya kuchangia. Naomba nianze kwa kushauri Wizara, Mheshimiwa Waziri na timu yake kwamba kuna haja kubwa sana sasa ya ku-diversify vyanzo vya utalii wetu na mapato ya utalii.

Waheshimiwa Wabunge wamezungumza mengi tangu Mheshimiwa Ally Saleh asubuhi na wengine wamegusia. Nchi nyingi duniani zinapata mapato makubwa kutokana na utalii wa historia tu, museums! Ukienda Vietnam War Museum in Washington DC, Lincoln Memorial, Washington Memorial, nenda kwenye museum za Ujerumani, nenda kwenye museum inaitwa Robben Island, it is a national park in South Africa. Mamia ya maelfu ya watalii wanakwenda sio kwa sababu kuna wanyamapori; wanakwenda kwa sababu kuna historia. Sasa sisi asilimia 90 ya mapato yetu ya utalii ni wanyamapori na tunajipongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, fikiria siku hawapo au mnafikiri wataendelea kuwepo milele. Fikiria hivi kuna siku hawapo, unafanya nini, fikiria! Kwa hiyo, hoja kubwa Mheshimiwa Waziri, think of diversification, weka mayai yako kwenye makapu mengi, kapu moja likianguka yatakayovunjika ni machache, hilo niliachie hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, haya masuala ya uhifadhi na mahusiano ya wananchi wanaoishi katika maeneo ya karibu na hifadhi zetu. Leo hii zaidi ya asilimia 30 ya total land mass ya Tanzania imehifadhiwa na maana yake nikwamba, wananchi kwa mamilioni wameondolewa kwenye maeneo hayo, wafugaji na wakulima hawapo. Namna pekee ambayo tumeitumia kwa miaka zaidi ya 50 ya kulinda maeneo haya ni kuyafanya kuwa maeneo ya kijeshi. Ndiyo maana katika sehemu kubwa yenye uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu kwenye Tanzania ya leo ukiachia vituo vya polisi ni kwenye maeneo ya hifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uhifadhi wa aina hii unaotegemea kutesa na kunyang’ana watu maeneo yao hauna future. Kuna siku hawa watu wataamka, watajibu halafu tutaenda wapi.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri naomba nisaidie tu, kuna sababu gani ya kisayansi leo ya kuwakataza wafugaji wa Kimasai ambao hawawindi kuchunga kwenye hifadhi walikofukuzwa mwaka 1959. Kama unataka kujua sayansi inasemaje soma Allan Rodgers na Kay Homewood 1995 – The Maasailand Ecology, wamesema maeneo haya ya uhifadhi yana wanyamapori kwasababu wafugaji wa Kimasai hawana shida na wanyamapori, sio wawindaji. Mmewafukuza mnawaharibia uchumi wao wa kiufugaji, siku wanyama wao wakiisha watakuwa wawindaji, wakipata bunduki kama Karamoja muone mtakwenda wapi na wanyamapori wenu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namna ya kuokoa long term, maslahi ya uhifadhi, namna ya kuwaokoa wanyamapori hawa na maeneo haya ni kuhakikisha kwamba zile shughuli za matumizi ya ardhi ambazo kihistoria hazina athari kwenye uhifadhi (pastoralism) zinakuwa integrated. Ngorongoro is a failure kwa sababu imekuwa undermined, the idea was good lakini imetekelezwa vibaya. Wamasai wa Ngorongoro leo ni maskini kuliko Wamasai wengine wote, sio kwa sababu Mungu amesema wawe maskini, ni kwa sababu yahii militarism katika conservation. Tunahitaji a new thinking, Mheshimiwa Mbunge wa Ngorongoro yuko hapa na sijamuona akizungumza, Wamasai wake…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lissu ahsante.