Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara ijikite katika kufanya tafiti mbalimbali kwa kushirikiana na Taasisi za Utafiti za Idara za Vyuo Vikuu na taasisi zingine zinazojihusisha na utafiti wa malikale au maliasili. Mpaka sasa bado Wizara haijajikita kiundani kuweza kuzigundua maliasili zetu nyingi tulizonazo hapa nchini hali inayopelekea Watanzania wengi kutokuwa na uelevu juu ya vivutio vya kale tulivyonavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ihakikishe inayatambua maeneo yote ya urithi wa kihistoria tuliyonayo hapa nchini na maeneo mengine yote yenye maliasili kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji na vitongoji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara kwa kushirikiana na Serikali kwa ujumla wahakikishe wanajenga miundombinu ya kufikia kirahisi maeneo yenye malikale na vivutio vingine vya asili ili paweze kufikika kirahisi na kujenga au kuweka karibu nyumba za kulala wageni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara ikishirikiana na Serikali katika kuanzisha utaratibu maalum wa kuwa na somo la ziada mashuleni ambalo litawafunza wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari pamoja na vyuo vikuu juu ya umuhimu na faida za malikale zetu na utalii tulionao hapa nchini.

Pia naiomba Wizara kuanzisha utaratibu maalum wa kuwapatia elimu wanavijiji na wananchi kupitia mikutano ya hadhara na mikutano mingine ya maendeleo ya vitongoji, vijiji na mitaa mijini. Ifikie mahali wananchi na wasomi wengi waone umuhimu wa kutembelea mali kale zetu mbalimbali walau kwa mwaka mara mbili, hii itapelekea kuongezeka kwa pato la ndani kupitia utalii wetu wa ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ihakikishe inayatambua maeneo yote ya urithi wa kihistoria tuliyonayo hapa nchini na maeneo yote yenye maliasili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali/Wizara ihakikishe kila panapofanyika ujenzi wa barabara itakayopita sehemu ndefu kuna mtaalam wa malikale na vivutio vingine vya asili ambavyo atavigundua na kushauri mradi huo usipite maeneo hayo upitie njia nyingine ili kuvilinda vivutio hivyo na kuvifanya kuwa hifadhi kwa manufaa ya Taifa letu.

Mheshimiwa Mwneyekiti, naunga mkono hoja.