Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Amb. Adadi Mohamed Rajabu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuchangia kwa kusema, naomba kuendelea kuchangia kwa maandishi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kuzuia kukata miti kwenye Hifadhi ya Msitu wa Amani naomba lipewe kipaumbele. Miti inakatwa na baadhi ya viongozi wa vijiji maeneo hayo wanasimamia, wanatumia misumeno ya chainsaw. Tumepeleka FFU mara mbili lakini wakiondoka tu kazi inaendelea wanaharibu vyanzo vya Mto Zigi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri humbly mhamishe kikosi cha wanyamapori kihamie moja kwa moja kupunguza gharama. Nakuhakikishia Mheshimiwa Waziri ukidharau usishangae msitu huu wa Amani ukaisha, hamishia kikosi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba uangalie uwezekano wa kusaidia Ofisi za Ubalozi wetu zenye uwezo wa kuleta watalii. Kuna wakati Wizara yako ilisaidia sana Ofisi zetu za Kibalozi na walisaidia sana kuwakilisha nchi mbalimbali ambazo mlishindwa kuhudhuria. Fikirieni kuweka fungu maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina uhakika kama njia na sehemu za kupumzika wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro, nilipopanda Mlima huo mwaka juzi hali ilikuwa mbaya. Naomba viboreshwe tafadhali.