Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. Martha Moses Mlata

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na pongezi kwa kazi nzuri sana inayofanywa na Waziri pamoja na Naibu Waziri, bila kuwasahau Katibu Mkuu na watendaji wote, naomba nitoe ushauri kidogo kuhusu suala ambalo ninaona; kuna utata na linatesa sana wazazi wa watoto wanaohitimu kidato cha nne.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtihani wa Taifa wa kuhitimu kidato cha nne hufanyika kila mwezi Oktoba ya mwaka, matokeo ya kidato cha nne hutoka kati ya Januari na Februari, lakini wanaopaswa kuendelea na masomo ya kidato cha tano wanasubiri hadi mwezi Julai. Hivyo, mtoto huyu ana miezi takribani nane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakika hii ni mateso sana kwa watoto kusubiri na wazazi kuwalinda watoto hawa ili wasije wakaingia kwenye kujifunza mambo yasiyofaa na kudumaza ari na moyo wa kusoma na uwezo unapungua. Hali hiyo, huwapelekea wale wenye uwezo kuwapeleka watoto wao pre-form five kitu ambacho kwa wasio na uwezo kinawanyanyapaa.

Ushauri wangu matokeo ya kidato cha nne yanatoka Januari ili kubaini waliofaulu, watoto wanaofaulu kuanzia alama ā€œDā€ one to three, wapelekwe JKT kwa muda wanaosubiria kuanza kidato cha tano mwezi wa saba. Hivyo, kuanzia Februari hadi Juni. Wakishahitimu watapata muda mdogo tu wa kukaa nyumbani na hivyo kuendelea na masomo vizuri. Hivyo itaondoa JKT ya kidato cha sita haitakuwa na haja ya kuwepo. Utaratibu wa kuwapata vijana kwenda kwenye Majeshi yetu unaotumika utabadilika na badala yake watapata walioenda JKT moja kwa moja. Mfano Jeshi la Polisi, Magereza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kama utaratibu wa kuwapeleka Jeshi la Kujenga Taifa litaonekana halifai, basi itafutwe namna yoyote kuhakikisha muda wa kuanza kidato cha tano unasogezwa ili waanze Mei.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hayo naunga mkono hoja.