Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Riziki Saidi Lulida

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kunijaalia nami kuchangia hoja iliyopo mbele yangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe shukurani za dhati kwa Mheshimiwa Ummy Mwalimu na Naibu waziri na Dkt. Mseru na Dkt. Mgassa. Mnamo mwezi Machi, kulikuwa na mtoto anaumwa sickle cell akawa na damu mbili nikapigiwa simu saa tano kwamba hali ya mtoto yule ni mbaya na huyo mtoto ni Rais wa ugonjwa wa sickle cell Africa. Nilimpigia Mheshimiwa Ummy usiku saa sita akanijibu na alitumia uwezo wake na huruma yake na yule mtoto aliongezwa damu, sasa hivi yule mtoto anaendelea salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, Dkt. Mgassa alikuwa nje ya nchi, baada ya kupata taratibu zile alimtafuta Dokta. mwingine ambaye alikuwa yuko Dar es Salaam mpaka saa 7.30 usiku yule mtoto ameweza kuongezewa damu lita kama nne hivi nafikiri na yule mtoto anatoa shukurani za dhati kwa niaba ya familia yake, Mheshimiwa Ummy na wote wahusika Mwenyezi Mungu awabariki sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nilikuwa mzima nikiwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano, nikapata ajali, sasa hivi mimi ni mlemavu. Mtu ambaye amenisaidia sana ni Dkt. Mseru Mwenyezi Mungu ambariki sana. Hivyo, kwa niaba ya Madaktari wote, naomba Dkt. Mseru anifikishie salamu zangu za dhati, Mwenyezi Mungu awajaalie Madaktari wote Tanzania kwa huruma na kazi ngumu wanazofanya kwa kuwasaidia Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ni Mwenyekiti wa kupambana na malaria ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mimi Riziki Said Lulida niko tayari kutokomeza malaria Tanzania wewe je? Twende zetu Kasulu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania tuna ugonjwa hatari wa malaria na malaria inaua, lakini nataka nitoe kitu kimoja ambacho nimekiona kwa muda mrefu kutokana na uzoefu niliokuwa nao. Malaria ni ugonjwa hatari lakini kuna wafadhili wanasema wao wanatoa fedha kwa ajili ya kusaidia malaria, hizi pesa hazionekani.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Waziri Mkuu kwa vile yeye ndio mdau katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Ummy Mwalimu na wenzake nataka watujibu hizi pesa za malaria zinakwenda wapi? Nimeweza kuhudhuria mikutano mingi ya mararia ikiongozwa na USAID na Taasisi nyingine wanasema tumepeleka Tanzania bilioni 600 zinakwenda wapi hizo pesa. Mimi sijajua mpaka leo na nimejaribu kumuuliza Naibu Waziri ananiambia hata na mimi vilevile Mheshimiwa Riziki hatujui pesa za malaria zinakwenda wapi.

Mheshimiwa Naibu Spika, malaria kama hizi pesa ambazo wanasema wanatuletea hazijulikani zinakwenda wapi, mimi napata kigugumizi na kujiuliza kuna nini na hizi pesa za malaria. Kwa mfano, pesa za UKIMWI zinaonekana ndani ya halmashauri, katika halmashauri tunaweza tukazikagua zile pesa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kuna hela za Global Fund, kuna hela za TACAIDS, kuna hela za Bill Clinton, Kuna hela za Foundation ya Benjamini Mkapa zinaingia ndani ya halmashauri na zinaweza kukaguliwa. Hizi pesa za malaria naomba Waziri mwenye dhamana aniambie ziko wapi ili tuweze kuzifanyia kazi na Watanzania waweze kuzitumia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, malaria yalikuwa yamepotea lakini sasa hivi malaria imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Mikoa ambayo ina malaria ni mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo Geita, Simiyu, Mara, Kigoma na Lindi na Mtwara. Sababu za msingi za kuwepo maeneo hayo malaria ni kwa ajili ya migodi mikubwa ambayo iko katika hiyo mikoa wameacha mahandaki makubwa, lakini mahandaki haya yalisababishwa na mikataba mibovu ambayo EIA haikufuatwa, hivyo baada ya kumaliza machimbo wameacha machimbo yakiwa wazi na mbu wamezaliana kwa wingi hiyo mikoa sasa hivi iko katika hatari kutokana na malaria.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba suala hili la malaria lisimamiwe kwa kikamilifu ili wananchi wa Mikoa hiyo Geita , Simiyu, Mtwara, Lindi, Kigoma, Katavi tutakuwa tumepoteza watu wengi hasa wanawake na watoto, wajawazito ndio walengwa wakubwa wa malaria.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitazungumzia suala la NHIF bima ya afya ni mkombozi kwa Watanzania na ilichukuliwa bima ya afya bima ikawa ni kwa ajili ya wafanyakazi wa Serikali na taasisi zake, lakini walisahau kama kuna wakulima wanauza mazao na hao wakulima wanapouza korosho wanapata pesa kama milioni 50 wengine milioni 20, naomba watu wa bima ya afya itengeneze mikakati maalum ya kuhakikisha hata wakulima na sekta binafsi ziwe zinatoa msaada na kuweza kulipia bima ya afya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini nazungumza hivyo Wabunge kila siku unapigiwa simu, mimi naumwa nataka kwenda Dar es Salaam lakini kama angetengenezewa mazingira mazuri ya korosho zake, kuwa unapouza korosho unatoa bima ya familia ya milioni 1,500,000, matatizo haya yangeweza kwisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna wavuvi wanavua kanda ya ziwa dagaa, Zanzibar wanavua kila kitu, wanapata pesa, je, ni mikakati gani wametengeneza ili watu wale wanawatembelea na kuweza kujiunga na bima ya afya. Mambo ya kuwa tegemezi kutegemea wafadhili, wafadhili sasa hivi wamekuwa kama wanatubabaisha, wanatunyanyasa leo nitatoa kesho sitoi. Mazingira haya ya kutegemea wafadhili ni aibu kwa Taifa tutumie njia ya sisi wenyewe kuweza kujitegemea na sio kutegemea watu wa nje. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeona tunaweza kutokomeza malaria kwa kutumia pesa zetu za ndani. Hatukatai kuchukua pesa za nje, lakini pesa za nje sasa hivi zina masharti ambayo yanatufanya tunakwazika, tunakuwa na madeni mengi ambayo tukijiuliza hela hizi kama hazisimamiwi, ni mzigo mkubwa kwa Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitazungumzia damu salama kwanza nataka nilete hamasa kwa Wabunge tuchangie damu salama. Ugonjwa wowote ni utarajiwa hautegemei wakati wowote, unaweza kupata ajali ukategemea upewe damu, unaweza ukajikuta mwanao anaumwa, familia yako inaumwa ,hivyo suala la damu salama lipewe kipaumbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, niwashukuru sana.