Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Janeth Maurice Massaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuongea; nitaongea kwa uchache sana. Sichoki na sichoki tena katika kumshukuru Mheshimiwa Rais wetu wa Awamu ya Tano kwa kazi nzuri anayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watakumbuka ndugu zangu, huko nyuma sisi tunaokwenda Mara tulikuwa tunapita Nairobi, Sirari ndiyo tunaingia Mara; wanaokwenda Kagera walikuwa wanapita Nairobi, Kampala huko ndiyo wanaingia kule Bukoba. Lakini chini ya uongozi tukimkumbuka Mheshimiwa Rais wetu ambaye alikuwa Waziri wa Ujenzi, hakulala, alikuwa analala kwenye mahema huko. Mheshimiwa Rais amejitoa muhanga katika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia siachi kumshukuru na kumpongeza, amefufua Shirika la Ndege, huko nyuma tulikuwa tunapiga kelele nchi haina ndege, nchi inaliwa, yeye amekuja ameleta ndege kwa mkupuo. Tunasema watalii wamepungua nchi hii hatuna alama, ameleta ndege ili tutangaze nchi yetu katika utalii. Mheshimiwa huyu amefungua barabara ukihesabu toka miezi miwili iliyopita hawezi kukaa wiki moja bila kufanya kazi, haijawahi kutokea Rais wa namna hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge, tusichoke kumuunga mkono. Kwanza ametupa heshima katika Chama chetu cha Mapinduzi, nawashangaa Wabunge wa Chama cha Mapinduzi ambao wanabeza mafanikio. Wengine wana hasira, kama hasira zako peleka nyumbani, lakini Chama cha Mapinduzi chini ya utekelezaji wa Ilani amefanya. Umpende usimpende, ndio Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza Mawaziri wake, wote wamemwelewa. Maana yake nikianza kumchambua Waziri wa Ujenzi, nikichambua Mawaziri wengine ambao bajeti zao zimepita, wote kila mtu anafanya kazi kwa bidii na umakini. Naibu Mawaziri wanakimbizana utafikiri panya, huyu katokea huku, huyu kaenda huku, mwingine analia, mwingine anabeba ndoo, wote wana lengo moja katika kujenga nyumba moja ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwapongeze Waheshimiwa Wabunge wa Upinzani, juzi wameunga mkono bajeti ya afya kwa asilimia mia, hongereni sana. Kwa sababu wanaelewa ukweli na sisi kama kwa wenzetu wamefanya kitu kizuri kwa kupongeza Serikali ya CCM basi na sisi tuwapongeze. Tunawapongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kero ndogondogo ambazo najua zitafanyiwa kazi, lakini kuna baadhi ya ma- engineer hawako makini. Kuna barabara za ndani za Mkoa wa Dar es Salaam, ni mbovu.

Waheshimiwa Wabunge, kusifia nitarudia bado naendelea! Maana yake hiyo inawachoma wengi!

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara za ndani za Mkoa wa Dar es Salaam ni mbovu. Kwa mfano, ukiangalia Barabara ya Segerea Seminari kuelekea Majumba Sita kupitia Kituo cha Polisi pale Stakishari, barabara ni mbovu, lakini hiyo barabara Mheshimiwa Rais aliahidi akiwa kwenye mkutano pale Vingunguti, tunamwomba Mheshimiwa Waziri aiangalie barabara hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Kinyerezi kwenda Malamba Mawili, tunaomba kasi iongezeke. Barabara tumeona imeharibika, Daraja la Kivule lile tunaomba pia kasi na umakini uongezeke; tunaomba ma- engineer wenye umakini waongezwe katika Mkoa wa Dar es Salaam maana kuna wengine hawako makini. Leo sipendi kuwataja watu, lakini kuna watu wanakera, tunaomba umakini katika kuangalia barabara zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile naomba Uwanja wa Ndege wa Musoma ujengwe.