Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. Dr. Jasmine Tiisekwa Bunga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Vyuo Vikuu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. DKT. JASMINE T. BUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nashukuru sana kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia katika Wizara hii ya Elimu. Niungane na Wabunge waliotangulia kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri pamoja na Watendaji wote katika Wizara hii ya Elimu kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya, bila kigugumizi tunaona mabadiliko makubwa ambayo yanatokea katika sekta yetu ya elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa miaka mingi tulikuwa tunalia na hizi shule kongwe Kilakala, Ilboru na zingine, mmeweza kuzikarabati ili sasa ziweze kuendelea kutoa elimu nzuri na mazingira mazuri kwa wanafunzi wetu tunashukuru sana. Pia katika usimamizi wa elimu bure kwa wanafunzi wetu shule ya msingi kuanzia Darasa la Kwanza mpaka form four tunapongeza sana Serikali. Pongezi kubwa ziende kwa Mheshimiwa Rais kwa kuweza kupitisha sera hii ya elimu bure moja kwa moja pale alipopata uongozi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nizungumzie zaidi na nijikite kwenye suala la ubora kwa sababu ukiangalia taarifa zote mbili, Wizara pamoja na taarifa ya Kamati zote kwa kweli kwa masikitiko inaonesha ubora wa elimu hasa shule za Serikali jinsi ubora wa elimu unavyozidi kushuka ndiyo maana watu hapa wanafanya comparison kati perfomarnce ya shule za private na shule za Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii pia kuwapongeza sana wadau wa shule za private wanafanya kazi kubwa sana, wanalenga hata fursa na soko la dunia hii linaendaje, hasa niwapongeze kwa kuweza kuipa kipaumbele lugha ya kiingereza katika taaluma. Kwa sababu hapa tunazungumzia lugha sawa kiswahili ni yetu lakini tunapozungumzia taaluma kwa sababu hii lugha ina mambo mengi ambayo ninaweza nikaeleza baadae. Nawapongeza sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala la ubora ubora huu wengi tumezungumzia hii performance, kuna factors ambazo zinafanya mwanafunzi afaulu, mioundombinu, walimu wa kotosha, motisha kwa walimu participation ya wadau mbalimbali wakiwemo wazazi, wanafunzi na lugha ya kufundishia, hivi ni vitu muhimu sana katika sekta hii ya elimu, lakini upande wa shule zetu za Serikali hizi factors zote zinasuasua zinayumba na ndiyo maana shule za private zina perfomance nzuri kwa sababu miuondombinu ni mizuri ya kufundishia, walimu wapo wa kutosha, motisha kwa walimu ni imporntant factor katika kufanya elimu bora wanapata, pia wazazi wako karibu sana na wanafunzi wao.

Ukiangalia kama walivyosema wachangiaji wengine hawa wanachukua wanafunzi wale cream ndiyo wako pale. Halafu na lugha ya kufundishia hao wanaanza toka chekechea mpaka form four wanatumia lugha ya kiingereza na ili mtu aweze kueleza ideas zake lugha ni muhimu sana, shule zetu za Serikali hivi vitu tuna-miss. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ushauri wangu ili shule za Serikali uonekane unafanya kazi boresheni miundombinu ya kufundishia. Sasa hivi tumeingia kwenye suala la elimu bure miundombinu haiko tayari, tatizo letu tunaanza ku-implement sera na kuifanyia kazi kabla ya maandilizi, hii ni changamoto kubwa sana kwa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano sasa hivi unasema watoto waishie darasa la sita mmefanya utafiti gani, mmewaandaa hawa watu kwa kiasi gani, mnachukua walimu wa sekondari mnawapeleka kufundisha Shule ya Msingi kweli wanafaa? Hivyo, hizi changamoto mzifanyie kazi ili siku moja na shule za Serikali tusimame kidedea. Ingawa kwangu nasema nakumbuka maneo ya Mwalimu Nyerere wakati anazungumza nchi matajiri na sisi ambao siyo, anakuambia unamchukua mtu wa heavy weight unaenda kumshindanisha na huyu wa featherweight haiwezekani huyu mwenye heavyweight atamshindwa. Kwa hiyo, hizi shule za private unazishindanisha na shule za Serikali moja kwa moja kati ya watu 100 Serikali itakuwa nne kutokana na ubora wa miundombinu na changamoto nyingine. Kwa hiyo Serikali muweze kuboresha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine nizungumze suala la lugha, kwamba lugha ni tatizo katika shule zetu. Mwanafunzi anaanza shule za Serikali zilizo nyingi kiswahili hadi darasa la saba, form one anaenda kiingereza hawezi kufanikiwa. Kwa hiyo, lazima tuchague lugha ya kiingereza ni rahisi kutengeneza vitabu vya kiada kuliko kule Chuo Kikuu. Chuo Kikuu ili mtu awe daktari alisomee sikio kwa wale ambao wamesoma degree mpaka Ph.D huko huwezi ukafanya utafiti kwa kutumia text book, unahitaji reference na bibliography, sikio lina vitabu zaidi ya 1,000 sasa wewe ukisema leo kwenye taaluma ukaweke lugha ya kiswahili hapana, hatutafika na fursa za dunia tutazikosa. (Makofi)

Mshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie kwa upande wa Vyuo Vikuu, nakupongeza sana suala la mikopo lilikuwa tatizo sasa hivi umejitahidi wanafunzi wetu wanaendea vizuri. Kwa hiyo, ninaomba sana kwa upande wa vyuo vikuu uweze kuboresha mambo yafuatayo:

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bima ya Afya kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, wanafunzi wanapofika term ya kwanza semester ya kwanza wanalipa zile fedha za bima, lakini baadae wanakuja kuipata semester ya pili, kwa hiyo, naomba uboreshe hiyo. Pia suala la kuhama chuo kutoka chuo kimoja kwenda chuo kingine bado mfumo hauko vizuri muufanyie kazi, kwenye mikopo ninataarifa kwamba wanafunzi 35 wa DIT wamepunguziwa ile ada ya mikopo kumetokea nini, badala ya shilingi 900,000 wanalipiwa shilingi 600,000 kumetokea nini? Mnawa-frustrate hawa wanafunzi. Vilevile muendeleze miundombinu kama hostel za wanafunzi ili kuwaokoa hawa... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.