Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo

Hon. Amb. Adadi Mohamed Rajabu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nashukuru sana kupata nafasi hii ya kuchangia kwenye hoja hii ya kilimo ambayo ni muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaposema kilimo kipewe kipaumbele ni muhimu sana, na ningeshauri kwamba kipaumbele hiki kiende sambamba na ujezni wa viwanda, tuwe wabunifu kwenye mambo mbalimbali yaweze kuweza kukuza kilimo chetu ili kumuondoa mkulima kulima na jembe. Sasa twende kwenye ubunifu wa ulimaji ambao ni wa kisasa, ulimaji ambao ni wa umwagiliaji, ambao utaleta manufaa makubwa kwa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa sana kuishauri Serikali kwamba kuna mifano mingi ya nchi nyingi, hili suala la mbolea, suala la mbegu, hebu Serikali ijiangalie, itoe mbegu bure, itoe mbolea bure. Tutakapotoa hivyo, kuna mifano ya nchi jirani ambayo imewahi kufanya hivyo, kwa hiyo nafikiri tutakapotoa hivi vitu bure na baadae tunakuja kuwachaji wakulima kwenye faida ambayo watapata baada ya kuuza hayo mazao yao. Nafikiri ni muhimu tuchague baadhi ya mazao ambayo tunaona kwaba yanaweza kuwa na manufaa kwa nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kule Tanga, Amani, tunalima sana chai, kuna kiwanda kimoja cha EUTCO, wanalima sana chai, lakini wana tatizo moja ambalo nimeshawahi kumwambia Mheshimiwa Waziri, kwamba hawa watu wanalima chai, wanatakiwa wa-brand, wanatakiwa wa-pack, wanatakiwa wauze, lakini hawaruhusiwi, wao wanalima baadaye wanaambiwa kwamba baada ya kuchakata wakauze mnadani kule Mombasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunawapa faida hawa watu wa Mombasa, watu wa Kenya, kwa nini hayo mambo tusiyafanye hapahapa nchini? Hawa watu wako tayari kabisa kufungua kiwanda, na ndiyo maana tunataka kwamba tuweke viwanda kwenye hii nchi viwe vingi. Sasa hivi vikwazo ambavyo vinawekwa hapa, naomba Mheshimiwa Waziri uliangalie sana hili, hii ni mara ya pili nakwambia, naomba uliondoe, waruhusiwe hawa watu, wachakate, wa-brand na wauze hapa hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni katani, naona vipaumbele vingi vinapewa kwenye korosho na pamba, lakini katani sasa hivi ina bei kubwa sana kwenye Soko la Dunia, lakini haipewi kipaumbele na sielewi ni kwa nini kwa sababu mashamba yametaifishwa lakini hakuna kiongozi ambaye anakuja kushawishi kuweza kusema kwamba tulime katani. Sasa naomba kabisa kwamba suala la katani lipewe kipaumbele, kwa sababu katani yenyewe si kamba tu, ina mambo mengi pale kwenye ule mti. Huwezi kutupa katani, inatengeneza mpaka umeme; kwa hiyo naomba kabisa kwamba Mheshimiwa Waziri suala hili la katani lipewe kipaumbele cha hali ya juu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri sana na ninaunga mkono Kamati ambayo imeshauri kwamba Mheshimiwa Spika na uzuri yuko hapa, atengeneze Kamati ya Bunge ambayo inaweza kushauri hili suala la kilimo, vinginevyo hatuelewi tunakwenda wapi, mbele, nyuma, bajeti inazidi kuteremka.