Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi. Niseme tu katikati ya Bunge kwamba nasikitika tu kwamba, kwa sisi tuliokuwepo Bunge liliopita kabla ya Bunge halijaanza tulikuwa tumepewa semina elekezi pale Blue Peal Dar es Salaam, kutenganisha mihimili hii mitatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi wakati mwingine sisi kama Wabunge tunasahau kabisa mhimili wetu una kazi gani dhidi ya Serikali. Kama Bunge lingekuwa linafanya kazi yake vizuri huu ndio wakati wa kuonesha power ya Bunge dhidi ya Serikali. Hii separation of power iliwekwa makusudi kwa sababu binadamu ana tabia ya ubinafsi, anataka yeye awe juu zaidi.

MheshimiMwenyekiti, kwa hiyo, ilivyowekwa Mahakama, Bunge na Serikali ni kuhakikisha yule anayeinuka zaidi avutwe mkia. Sasa kwa bahati mbaya Bunge letu tunadhani Serikali ina nguvu kuliko sisi. Ndio maana Wabunge wengi hapa wanapiga magoti na kuombaomba wakati Serikali kimsingi kupitia Waziri wa Fedha imekuja hapa kutuomba sisi tuidhinishe kutumia matumizi hayo. Ni wakati huu ambao Bunge lilitakiwa liiadabishe Serikali kwa matumizi ambayo Bunge halikuidhinisha. Sasa kwa sababu hatujui nguvu ya Bunge tumekuja hapa tunajibembeleza na naomba zahanati, naomba dispensary, naomba Kituo cha Afya wakati haya mambo ndio wakati wa Bunge kusema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wajibu wa Wabunge kujua what is our power, nguvu zetu ni zipi? Ndio maana CAG amekuja hapa ambaye ni jicho la Serikali, ni jicho la Bunge. Yeye ni Mkaguzi baada ya Serikali kuomba ruhusa ya kutumia pesa, sisi hatuna uwezo wa kwenda kukagua huko, CAG amekwenda kukagua kwa niaba yetu, anakuja anasema nimeona hili, nimeona hili halijapangwa vizuri, Wabunge wengine hapa wanamlaumu CAG. Ignorance ya kujua wajibu wetu kama Wabunge na hii tuna li-cripple Bunge tunasababisha watu wengine ambao ni wabinafsi wakue zaidi kuliko Bunge linavyotakiwa liwepo. Niwaombe ndugu zangu na nimpongeze Mheshimiwa Kadutu amefanya kazi ya Kibunge bila kujali itikadi za vyama kwa matatizo tuliyonayo kwenye majimbo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nakuja kwa Mheshimiwa Dkt. Mpango; mara tu alivyochukua Uwaziri alipoanza hapa alikuwa anahutubia kama yupo kwenye Lecture room, alikuwa kinadharia sana. Tulikwambia this is not a lecture room, sisi tupo kwenye ground. Tunakutana na watu, tunaishi na watu, hizi kodi ambazo leo amezitoa we told you three years back, kwamba hizi kodi zitaleta matatizo kwenye uchumi you never listen. Sasa hivi amerudi kwenye mgongo mwingine, halafu Wabunge hapa wanasema tunampongeza, tunaipongeza Serikali, yeye ndiye alitupeleka kule. Bado tunaendelea kusisitiza, huu utaratibu wa uchumi unaokwenda sasa hivi, huko mbele tunakwenda ku-crush na utaweka historia tunakwenda ku-crush kwa sababu uchumi tunaokwenda nao sio halisia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, asubuhi Mheshimiwa Sugu amesema hapa sisi tunaozungumza, najua Mheshimiwa Rais anasikia, actually sisi ndio tunaompenda Rais kuliko wengi wenu huko. Kwa sababu wanampaka Rais kwa mgongo wa chupa hawamwambii ukweli. They economy going crush kwa sababu huwezi kuniambia uchumi unakuwa, toka Serikali ya Awamu ya Tano nimeingia kwenye jimbo langu akinamama wale wengine wameuziwa fridge au wamenyang’anywa, wamenyang’anywa television na makochi kwa sababu hawawezi kulipa mikopo. Sasa utaniambiaje uchumi unakua kwa sababu hawawezi kufanya business, uchumi haukui.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka nimuulize swali Mheshimiwa Mpango, naomba anijibu honestly, Serikali ya Awamu ya Tano inaendesha hii nchi utadhania sisi ni Sudan ya Kusini, trial and error ambayo imezaliwa juzi. Serikali hii haina consistency kwa sababu nchi hii tokea tumepata uhuru ni Chama cha Mapinduzi kimekuwa kikitawala. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakubaliana wakati wa Mwalimu Nyerere kuna makosa mengine aliyafanya aliendelea kurekebisha kwa mfano hizi Serikali za Mitaa aliwahi ku-centralize akaona makosa akarudisha. Tunaweza tukamsamehe kwa sababu ndio kwanza tulikuwa tunapata Uhuru, lakini alivyokuja Mheshimiwa Mwinyi tukahama direction, tukahama mwelekeo, tukaacha mambo ya ujamaa, tukawa na free market katika nchi hii. Alivyokuja Mheshimiwa Mkapa naye akaanza, tukaanza kuweka wawekezaji akatengeneza mazingira ya wawekezaji tukaanza kuwa friendly kwa wageni ambao tuliwafukuza mwanzoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, amekuja Mheshimiwa Dkt. Kikwete ametengeneza mazingira mazuri ya kuwa na marafiki wa nje, kuwafanya investors waje. Sasa swali kwa Mheshimiwa Dkt. Mpango aniambie namwona hapa wakati wa Mheshimiwa Kikwete alikuwa Katibu wa Tume ya Mipango ambayo sasa hivi unataka kuifuta. Wakati wa Rais Mheshimiwa Dkt. Kikwete, Mheshimiwa Dkt. Mpango alisimamia Kilimo kwanza, alisimamia SAGCOT, alisimamia Big Results Now, alisimamia Gesi, alisimamia PPP na wali- encourage D by D. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kwenye Awamu ya Tano amegeuka, ameenda kwenye mambo ya Stiegler’s Gorge, kwenye Standard Gauge ambayo mikopo yote hii anaichukua sio concessional loans, anachukua mikopo ambayo ni ya gharama kwa nchi hii, tell us wewe ni mchumi unayeamini nini? Atuambie hapa uchumi ule aliokuwa anaendesha Mheshimiwa Dkt. Kikwete ambaye alitengeneza mazingira mazuri ulikuwa na makosa au alimuingiza chaka? Sasa hivi ameweka u-turn, where are we heading as a Nation? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchumi wakati wa Serikali ya Kikwete ulikuwa una-embrace investors, ulikuwa una mazingira mazuri ya kuwaleta wawekezaji. Uchumi huu unagombana na wawekezaji, wanaonekana wote wizi katika uchumi huu ambao yeye ndiye Waziri. Wafanyabiashara wote wanaonekana ni wezi, wafanyabiashara wanaonekana hawalipi kodi, atuambie ni uchumi upi ambao anauamini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais wetu yeye sio mchumi, ni engineer, tunategemea Mheshimiwa Waziri ambaye ni Mchumi ampe maekelezo mazuri ambayo yatasaidia nchi yetu iende. Leo naongea kwa masikitiko makubwa kwa sababu tunaua Local Governments kwa uchumi wa namna hii, vyanzo vyote amechukua kwenye Local Government anavileta Central Government kuna maumivu makubwa ambayo yanapatikana kwenye Local Government. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Dkt. Mpango atoe majibu ni uchumi upi anauamini, what do you believe as an economics? Nani anamdanganya kati ya Mheshimiwa Dkt. Kikwete na Rais wa sasa? Kwa sababu Mheshimiwa Dkt. Kikwete alitengeneza mazingira pamoja na udhaifu wa Serikali ya Awamu ya Nne, alitengeneza mazingira mazuri ya kuwa na mahusiano na watu wa nje, alileta wawekezaji kulikuwa na mazingira mazuri, leo haya yoote umeyakataa, leo uko kwenye… (Makofi)

T A A R I F A . . .

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, namtaka Mheshimiwa Dkt. Mpango aniambie kichumi, nimesema wakati wa Mheshimiwa Dkt. Kikwete yeye alitu- encourage kwenye mambo ya SAGCOT, SAGCOT inazungumza kuhusu umwagiliaji kwamba tumwagilie, Stiegler’s Gorge inataka bwawa lile lijae. Sasa ni kwa namna gani tunaweza tukatekeleza SAGCOT na wakati huo huo tukaenda na Stiegler’s Gorge kwa maji yaleyale, ambayo upande wa SAGCOT tunataka tumwagilie kwenye kilimo cha umwagiliaji na wakati huo huo tunataka bwawa la umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ndio mambo ambayo kama Bunge tunatakiwa tujadiliane bila kujali itikadi za vyama. Nasema tutapigana makofi hapa lakini the economy is sinking na tunakwenda ku-crush sio muda mrefu kwa sababu tunakopa mikopo ambayo ni gharama kubwa. Makusanyo ni trilioni kumi na nne tu na bado tunaenda kwenye negative, hatuna hiyo pesa naomba Mheshimiwa Dkt. Mpango na juzi nilimuuliza kwenye Wizara yake kwamba ni kiasi gani cha pesa ambacho ni cha TRA. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, dada yangu Mheshimiwa Dkt. Sware amezungumza hapa hela zote ambazo wanadaiwa hizo ni kiasi gani ambacho wanakusanya kwenye TRA, lakini tukija hapa tunapongezana pongezan. Huu ndio wakati wa kuonesha the power of the Parliament. Tulitakiwa tushikamane kwamba ni kwa nini Serikali hii inalikosea adabu Bunge?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuuliza kwa nini Serikali inafungua miradi ambayo Bunge halijapitisha. Inaanza kuanzisha halafu tumekaa hapa tunapigania makofi kwa sababu Serikali ikileta maji kwenye jimbo langu is not a fever am the tax payer representative, mimi nawakilisha wapiga Kura wangu kule, kwa hiyo, siwezi kumpigia magoti Mheshimiwa Dkt. Mpango hapa. (Makofi)

T A A R I F A . . .

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekikti, Serikali ya Chama cha Mapinduzi is crying for my endorsement, am smart enough, nikitaka kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Magufuli naweza kuchukua TBC au ITV. Msiwe mnaviziavizia ndio nasema hapa simpongezi hapa ndio nasema sasa simpongezi kwa sababu ana washauri ambao mnampotosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi huko nje wanalalamika, there is no money kwenye mifuko, haya ndio ya kujadili kama Bunge, wengi huko mitaani kwenye majimbo yetu mimi saa hizi ukienda jimboni kwangu file la mahitaji liko hivi. Limekaa hivi, sijasoma nahitaji mtoto shule, ada, sijui nini, mafaili makubwa yamejaa hivi, hata mimi mwenyewe sina hela na nyie wenyewe ndio hayohayo, halafu tukija hapa tunadanganyana. Tuoneshe nguvu ya Bunge wewe mwenyewe Mheshimiwa Jenista unalalamika huna hela, tukikaa, saa hizi tuanze kukaa tunadanganyana tunapongezana, hakuna hela, huu uchumi Mheshimiwa Spika amezungumza asubuhi hapa uchumi kila mtu anao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema juzi I am a theologian by profession, lakini huwezi kuniambia kwamba siwezi kuguswa kama hamna hela! Hata mama kule nyumbani anajua kama uchumi umekaa vibaya, uchumi haupo, tusidanganyane hapa, haukui! Wazimbabwe wanasema mtoto ambaye analia njaa leo huwezi kumwambia jana nilikupa chakula. Hakuna chakula huko mitaani tusidanganyane hapa hakuna chakula, hayo mambo ya ndege, kwanza ndege wametuletea disaster, wanapata hasara halafu hawasemi hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ni mambo lazima tujadili kama Bunge na lazima tuoneshe power kwa Mheshimiwa Dkt. Mpango kwamba lazima awajibike. Hela ambazo ametumia bila kupata vibali vya Bunge anatakiwa awajibike. Sasa tumekaa hapa tunapongezana ametumia hela nyingi bila kibali cha Bunge, sasa Bunge lina kazi gani? Vinginevyo Bunge limemezwa, linawafanya wale watu wabinafsi wainuke zaidi.