Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Hon. Anna Richard Lupembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nsimbo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa naomba nipongeze kazi nzuri sana ya Serikali ya Awamu ya Tano na Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa sana ambazo anafanya kwa Watanzania. Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Mawaziri, hongereni sana kwa kazi nzuri ya kujenga nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna changamoto chache za shule za msingi hususan madarasa pamoja na matundu ya vyoo. Naomba sana Serikali ielekeze mpango mkakati kwa ajili ya mambo muhimu sana hayo kwa ajili ya watoto wetu ili waweze kusoma vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Walimu wetu ni wachache sana hususan vijijini pamoja na wahudumu wa zahanati zetu, Manesi, Madaktari, Watendaji wa Vijiji, Kata vilevile kada ya kilimo na Maendeleo ya Jamii. Tunaomba sana Serikali iweke nguvu katika maeneo hayo kwa sababu ndio wanaosimamia maendeleo yetu katika vijiji vyetu pamoja na kata zetu kwa ajili ya wananchi kwa ajili ya huduma mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maji vijijini bado wananchi wa Mkoa wa Katavi kupitia vijiji vyake maji bado shida sana. Huo ndio ushauri wangu. Ahsante.