Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Hon. Alfredina Apolinary Kahigi

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

MHE. ALFREDINA A. KAHIGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza na pongezi. Sina budi kuipongeza Wizara ya TAMISEMI, Waziri Jaffo, Naibu Mawaziri wake, Mheshimiwa Kakunda na Mheshimiwa Kandege pamoja na Makatibu wao wote kwa kazi zao nzuri na usikivu wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini tumepewa milioni 900 za force account na Serikali. Fedha hizi tumezigawa katika kata mbili; Kata ya Katoro milioni 500 na Kata ya Kishage milioni 400. Katika Kata hizo wanajengewa nyumba za mama na mtoto, nyumba za Waganga kila kata nyumba moja moja na mochwari moja moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo, tuna shida ya Wahandisi wa Ujenzi, tunaomba Serikali itusaidie wahandisi hao maana Wahandisi wa kujitegemea gharama zao ni kubwa sana. Tuna Wahandisi wa TARURA tukiwaomba wanasema wao ni wa barabara. Tunaomba sana watuonee huruma katika shida hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru zahanati tunazo, vituo vya afya angalau tunavyo na dawa zipo, shida hatuna Manesi, pia na Waganga ni wachache sana, tunaomba na eneo hilo tusaidiwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu; tuna shida sana na Walimu wa shule za msingi na sekondari kwani tuna upungufu sana. Vile vile tusaidiwe nyumba za Walimu ni shida, vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunamwomba Mheshimiwa Waziri katika bajeti yake, basi aiangalie Wilaya yetu ya Bukoba Vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haya machache, nashukuru.