Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nachukua nafasi hii kukushukuru wewe kwa kunipa fursa hii ya kuchangia katika hotuba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Pili, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kuandika na kuiwasilisha kwa ufasaha hotuba hii. Katika kuchangia hotuba hii, napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, upimaji wa viwanja na mashamba; napenda kuipongeza Wizara kwa hatua yake ya kuendelea kupima na kuwapatia viwanja vya makazi wanachi wetu ili kuwaondolea matatizo ya uhaba wa viwanja. Makazi ni hitaji muhimu sana katika maisha ya mwanadamu lakini inaonekana kuwa bado bei ya viwanja si rafiki kwa wananchi wa kawaida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bei ya viwanja ni kubwa sana kiasi ambacho wananchi wanakata tamaa na na hivyo kusababisha wananchi hao kutafuta njia mbadala ya kujikatia maeneo ya makazi kwenye maeneo yaliyo karibu nao, jambo ambalo linapelekea kuharibu azma na mpango mzuri uliowekwa na Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu katika jambo hili ni kuiomba Wizara kupunguza bei ya viwanja hasa vya makazi ili kuwawezesha wananchi kumudu gharama hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.