Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017

Hon. Hafidh Ali Tahir

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dimani

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017

MHE. HAFIDH ALI TAHIR: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kusema machache kutokana na hotuba hii ya Waziri inayohusu Katiba na Sheria. Ninampongeza Waziri kwa yale yote ambayo yameelezwa katika kitabu chake na mimi kama mmoja wa wadau wa kitabu hiki basi napenda nimshukuru sana.
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri kama kawaida atika Bunge letu siku hizi huwa kuna hotuba ya Waziri na ile ya Kambi ya Upinzani. Tunaziangalia na tunazisikiliza nilikuwa nikisikiliza sana hotuba ya Mheshimiwa wa Kambi ya Upinzani, na nimekwenda kwenye ukurasa wa nane wa kitabu chake, hali kadhalika nimesogea katika ukurasa wa tisa, yale ambayo yamezungumzwa humu, ni mambo ambayo tulikuwa tunakumbushana tu.
Mheshimiwa Spika, kwa sababu ukiangalia ukurasa wa nane kuna suala kwamba limezungumzwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano kazumgumzwa Rais wa Zanzibar katika Jamhuri ya Muungano, sote tunafahamu hivyo na tumefahamu hivyo kwa sababu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Katiba yake inasema wazi kwamba kutakuwa na Serikali mbili ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Moja ya Zanzibar na ile ya Muungano. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pia Katiba hiyo inasema kutakuwa na Maraisi wawili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mmoja wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hivyo ndivyo Katiba ilivyosema wala hatuna haja ya kukumbushana kwa sababu sote tunajua, wala sikuona faida ya kuandikwa kwenye kitabu hiki kwa sababu ni jambo la kawaida.
Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa tisa kuna mtu mmoja ametangazwa anaitwa Ghassany katika kitabu chake, amezungumzia kuhusu Kwaheri ukoloni, kwaheri uhuru wa Zanzibar na karibu Mapinduzi. Hatuna haja ya kukumbushana, kwa sababu aliyeandika kitabu hiki alijua kwamba baada ya Mapinduzi, ukoloni kwaheri, alikuwa anajua kwamba baada ya Mapinduzi, na wale waliotawala pia kwaheri, lakini yakakaribishwa Mapinduzi!
Mheshimiwa Spika, haya ni mambo ya kawaida na mimi namshukuru sana Kiongozi wa Kambi ya Upinzani kwamba na haya anayafahamu. Lakini lingine ambalo limezungumzwa hapa na wenzetu wa Kambi ya Upinzani, wanasema kwamba Tanganyika, wametumia neno Tanganyika, siyo vibaya! wametumia neno Tanganyika kwamba ilishiriki kikamilifu katika Mapinduzi ya Zanzibar hakuna asiyejua katika ulimwengu huu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Wanzanzibar tunajua kwamba Mapinduzi ya Zanzibar yamechangiwa sana na ndugu zetu wa Tanganyika, yalichangiwa kwa sababu maalum, siyo kwa kubahatisha hapana! Juzi nilisema hapa mimi waliokwenda Zanzibar hawakutokea Dubai, walioanzisha Kisiwa cha Zanzibar hawakutoka Oman, walioanzisha Kisiwa cha Zanzibar hawakutoka Qatar, walioanzisha Zanzibar wametoka Bagamoyo, wametoka Tabora, wametoka Mtwara na sehemu nyingine.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, hawa ndiyo walioanzisha Zanzibar, miongoni mwa hao walioanzisha Zanzibar wengine humu babu zao wamo, sasa mimi nashangaa sana kusema kwamba Tanganyika imesaidia kweli Tanganyika imesaidia Mapinduzi ya Zanzibar, itaendelea kusaidia Mapinduzi ya Zanzibar wakati huu Tanzania.
Mheshimiwa Spika, wamesaidia tumeweka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wanaendelea kusaidia Zanzibar, wataendelea kusaidia Zanzibar kwa maana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na atakayejaribu kuigusa Zanzibar atajua Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ipo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sisi tumepindua kuondoa ukoloni, na tunaendelea kulinda Mapinduzi makusudi wala hatuwezi kumpa nafasi, mtu ambaye ana uchu wa madaraka haiwezekani. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tumekuwa na viongozi wengi pale walafi wa madaraka wengi tu, lakini tumekuwa na viongozi wengi ambao wanatumwa siyo mara moja, siyo mara mbili kuna historia pale ya Mapinduzi yaliyokuwa yanataka kufanywa Zanzibar mara 23, majaribio ya Mapinduzi hayakufanikiwa! Hayakufanikiwa kwa sababu Muungano wetu uko imara na hatuwezi tukampa mtu madaraka mwenye ulafi.
Mheshimiwa Spika, nitawapa mfano hai tu, hapa wenzetu wanazungumza sana na juzi nimemsema Maalim, sawa Maalim lakini kwa Zanzibar Maalim ni Maalim tu na kwa sababu tumekaa naye Maalim tunajua Maalim yukoje.
Mheshimiwa Spika, rafiki yangu leo bahati mbaya Mheshimiwa Ally Saleh hayupo hapa, Maalim alikuwa anasoma Lumumba, pale Lumumba palikuwa na timu ya mpira, palifanyika uchaguzi wa uongozi wa timu ya mpira Maalim aligombea ukapteni, lakini hachezi. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Spika, haiwezekani! Hiyo ndiyo dira iliyotuonesha Maalim yukoje, utakuwaje kepteni wa mpira wewe mwenyewe huchezi? Haiwezekani, kwa sababu alitaka na yeye awemo akagombea ukepteni watu wakampa, watu wanakwenda Lumumba kucheza yeye amekaa nje, kepteni huyo? Hilo ni matatizo. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Spika, siyo hilo tu, tunapokaa tukasema Mapinduzi tutayalinda, tutayalinda kweli na tutawapa watu wanamapinduzi.
MHE. HAFIDH ALI TAHIR: Tutalinda kwa Jeshi, tutalinda kwa Polisi, tutalinda kwa chochote, hii ndiyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninyi mmepata kuona wapi Mapinduzi yakalindwa kwa kanga, utalinda Mapinduzi kwa kanga? Mapinduzi tumepindua tumekwenda Jeshini tukachukua mashoka tukalinda na tutaendelea kulinda.
Mheshimiwa Spika, nabaki hapa kwenye kiongozi mlafi hatuwezi hata wale ndugu zangu Wapemba tukitembea kule huwa wanatuambia kwa lugha ile ya kwao kipemba. Hivi mwataka kumpa Urais mtu asiye nyumba kwao au ugenini? Umesikia lugha? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, huwezi kuwa Rais kama huna mke haiwezekani, umepata kuona wapi? Unataka tukupe nchi huna nyumba, haiwezekani!
MHE. HAFIDH ALI TAHIR: Kwa hiyo, tunachosema Mapinduzi ya Zanzibar yatalindwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tena yatalindwa kwa nguvu zote. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, juzi nilikuwa nazungumza suala la Serikali ya Umoja wa Kitaifa jinsi ilivyokuja Zanzibar, kila mtu Mzanzibar anajua, mpaka hawa ndugu zetu hawa wanajua, imekujaje Serikali ya Umoja wa Kitaifa kama juzi nilivyotoa mfano nasema walikaa watu wawili wakazungumza peke yao, CUF wanashindwa kumuuliza Maalim Seif umezungumza nini na Mheshimiwa Amani mtoto wa Mama Fatma? Wanashindwa kumuuliza, waulize mpaka leo!
Mheshimiwa Spika, hiyo haitoshi imekuja Serikali ya Umoja wa Kitaifa wakati wa kampeni, unaleta posters zinasema Ally Hassan Mwinyi anasema ndiyo, Mkapa anasema ndiyo, wewe unasemaje, huyo Mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi kaulizwa lini? Hajaulizwa wanasema Salmin anasema ndiyo kaulizwa lini na mwenyewe akasimama akasema hamjaniuliza, lakini Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa sababu siyo Maalim juzi kawafanya kitendo hawa, kawafanya kitendo kibaya sana, kwa sababu kajua kama akienda hospitali atalipwa milioni 350, halafu atasema kwamba uchaguzi hawa wasiende, hawakuenda katika uchaguzi, mambo ya ajabu sana……….
MHE. HAFIDH ALI TAHIR: Mheshimiwa Spika, Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekufa. Naunga mkono hoja.