Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 7 Sitting 19 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 156 2017-05-08

Name

Josephine Tabitha Chagulla

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHINE T. CHAGULA aliuliza:-
Serikali ilipandisha hadhi Kituo cha Afya Kharumwa kuwa Hospitali ya Wilaya Nyang’hwale.
Je, ni lini Serikali itaongeza majengo kwa ajili ya wodi
za wagonjwa na wodi za wazazi katika hospitali hiyo?

Name

Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MITAA SERIKALI ZA MIKOA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Josephine Tabitha Chagula, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017, Halmashauri ya Wilaya ya Ngang’wale ilitengewa ruzuku ya maendeleo isiyokuwa na masharti (LGDG) kiasi cha 533,822,000 kwa ajili ya ujenzi wa miradi, ikiwemo sekta ya afya. Kati ya fedha hizo shilingi milioni 186.6 zimeshapokelewa. Fedha hizo zinapaswa kutekeleza miradi ambayo ni kipaumbele cha halmshauri kilichowekwa na wananchi wenyewe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imeongeza ruzuku ya maendeleo hadi shilingi bilioni 1.038 sawa na ongezeko la asilimia 95. Vipaumbele vya matumizi ya fedha hizo ikiwemo ujenzi wa wodi, vitapangwa na halmashauri zenyewe kwa kuzingatia fursa na vikwazo vilivyopo.