Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 8 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 68 2017-09-12

Name

Lolesia Jeremia Maselle Bukwimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Busanda

Primary Question

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itawalipa walimu madai yao ya kusimamia mtihani wa kidato cha nne mwaka 2015 na mtihani wa kidato cha pili mwaka 2016?

Name

Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lolesia Jeremiah Bukwimba, Mbunge wa Busanda, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, walimu waliosimamia mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka 2015 wanadai jumla ya shilingi bilioni 1.6 na walimu waliosimamia mitihani ya kidato cha pili mwaka 2016 wanadai jumla ya shilingi bilioni 3.2. Hivyo, jumla ya madai kwa mitihani yote miwili ni shilingi bilioni 4.89.
Mheshimiwa Spika, madeni hayo yamewasilishwa Hazina kwa ajili ya uhakiki ili walimu hao wapewe madai yao.