Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 18 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 1 2020-01-28

Name

Livingstone Joseph Lusinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtera

Primary Question

MHE. LIVINGSTONE J. LUSINDE aliuliza:-

Je, ni lini barabara ya Mvumi Mission itajengwa kwa kiwango cha lami?

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, nakushukuru na kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Livingstone Lusinde, Mbunge wa Mtera kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Barabara wa mwaka wa fedha 2019/2020 imetenga kiasi cha shilingi milioni 375 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Mvumi Mission kwa kipande chenye urefu wa kilometa moja kwa kiwango cha lami. Maandalizi ya ujenzi yameshaanza na ujenzi unatarajia kukamika ifikapo mwezi Agosti, 2020.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja katika Jimbo la Mtera kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. Ahsante.