Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 19 Sitting 3 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 24 2020-04-02

Name

Jaku Hashim Ayoub

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. JAKU HASHIM AYOUB aliuliza:-

Kituo cha Polisi cha Malindi kilichopo Unguja ni kituo cha kihistoria na cha mfano, lakini kituo hicho tangu kimejengwa na wakoloni hakijawahi kufanyiwa ukarabati na kwa sasa kiko taabani:-

(a) Je, ni lini Kituo hicho kitafanyiwa ukarabati?

(b) Je, ni bajeti kiasi gani inahitajika kwenye ukarabati wa kituo hicho?

(c) Je, Serikali haioni kuwa kituo hicho kitavunjiwa hadhi yake ya kihistoria?

Name

Kangi Alphaxard Lugola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jaku Hashim Ayoub, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, jengo linalotumika kama Kituo cha Polisi Malindi ni moja ya majengo ya zamani yaliyojengwa enzi za mkoloni ambayo yanasimamiwa na Idara ya Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe ambayo inapata msaada kutoka Shirika la UNICEF. Jeshi la Polisi linashirikiana na wataalamu wa Idara ya Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe kuona ni namna gani ukarabati wa jengo hilo utafanyika kwa kuzingatia Sheria ya Uhifadhi na kuendeleza Mji Mkongwe.

Mheshimiwa Spika, tathmini ya ukarabati wa jengo hilo inatarajiwa kufanyika hivi karibuni baada ya makubaliano ya wataalamu wa Jeshi la Polisi na wataalamu wa Idara ya Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe.

Mheshimiwa Spika, ili kulinda historia ya jengo hili taratibu na kanuni za Idara ya Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe zitafuatwa na kutekelezwa.