Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 2 Sitting 6 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 86 2021-02-09

Name

Daimu Iddi Mpakate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kusini

Primary Question

MHE. DAIMU I. MPAKATE Aliuliza :-

Jimbo la Tunduru Kusini limepakana na Nchi ya Msumbiji kwa upande wa Kusini.

Je, ni lini Serikali itajenga Kituo cha Uhamiaji na cha Polisi kuhudumia maeneo hayo ya mpakani?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI Alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Daimu Iddi Mpakate, Mbunge wa Tunduru Kusini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, jitihada za ujenzi wa Kituo cha Polisi daraja ā€œCā€ unaofanywa na Halmashauri ya Tunduru umefikia katika hatua ya lenta. Aidha, ujenzi wa Kituo cha Uhamiaji utategemea makubaliano baina ya Serikali ya Tanzania na Msumbiji kama taratibu za ujenzi wa Vituo vya Uhamiaji mipakani unavyotaka. Kwa sasa makubaliano hayo bado hayajafanyika.