Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 4 Sitting 5 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 61 2021-09-06

Name

Maryam Azan Mwinyi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Chake Chake

Primary Question

MHE. MARYAM AZAN MWINYI Aliuliza: -

Je, Serikali haioni haja ya kuwa na Mtaala mmoja kuanzia Kidato cha Kwanza hadi cha Nne kati ya Tanzania Bara na Zanzibar? (Makofi)

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA Alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Maryam Azan Mwinyi Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikishirikiana vizuri na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo suala la elimu hususan katika utekelezaji wa mitaala na kutoa elimu bora kwa watoto wa kitanzania.

Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa mitaala ya elimu kati ya Tanzania Bara na Visiwani, pande zote mbili hutumia mtaala mmoja kuanzia Kidato cha Kwanza hadi Kidato cha Sita. Ahsante.