Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Augustino Manyanda Masele

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbogwe

Primary Question

MHE. AUGUSTINO M. MASELE aliuliza:- Leseni ya utafiti wa uchimbaji wa dhahabu ya Mabangu imechukua muda mrefu sana katika Kata za Nyakafuru na Bukandwe. Je, ni lini mgodi wa uchimbaji dhahabu baina ya Mabangu na Resolute utaanza uzalishaji?

Supplementary Question 1

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi ili niweze kumuuliza swali Mheshimiwa Naibu Waziri.
Kwanza, kwa sababu Kampuni ya Resolute imeamua kuachia leseni zake tisa, je, Serikali itakuwa tayari sasa kuzigawa hizo sasa leseni kwa wachimbaji wadogo Wilayani Mbogwe ili waweze kunufaika na dhahabu iliyopo katika eneo hilo? (Makofi)
Swali la pili, dawa ya deni ni kulipa. Kampuni hii ya Resolute inadaiwa sasa shilingi bilioni 143 na Serikali. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha kwamba deni hili linalipwa kwa wakati? (Makofi)

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa Mheshimiwa Masele nakupongeza sana, najua juhudi zako na wananchi wako wanatambua jinsi unavyoshughulikia maslahi ya wananchi hasa wachimbaji wadogo.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza ni kweli kabisa tumejadiliana sana na kampuni hii, kampuni hii ina leseni 22 na maeneo mengi haiyafanyii kazi, kwa hiyo tumekubaliana na Kampuni hiyo sasa imeamua kuya-surrender maeneo tisa na maeneo hayo tunagawa sasa kwa wananchi wa Mbogwe, Mheshimiwa Mbunge ninakushauri sana sasa wananchi wako waanze kuunda vikundi ili sasa waweze kurasimishwa, mpango wa kuwagawia ifikapo mwezi wa Julai na Agosti, tutawamilikisha rasmi.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na deni, ni kweli kabisa dawa ya deni ni kulipa. Kampuni hii imekuwa ikidaiwa shilingi bilioni 143.007 na kwa sababu ilitaka kuhamisha umiliki wake sisi Serikali tulikataa mpaka deni litakapolipwa.
Mheshimiwa Spika, sasa hatua inayofanyika wamekubaliana na TRA na Kampuni imekubali kulipa, kwa hiyo kuja kufika mwezi wa Julai, kampuni imeahidi kulipa deni hilo. Baada ya kulipa sasa taratibu za umilikishaji zitaendelea rasmi.