Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Yosepher Ferdinand Komba

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza:- Katika Mpango wa Kilimo Kwanza Serikali ilihamasisha Watanzania kuongeza uzalishaji katika kilimo ili Serikali itoe mikopo ya matrekta kwa wingi. (a) Je, kumekuwa na mafanikio kiasi gani kwa mazao ya biashara na chakula? (b) Kama kumekuwa na mafanikio, je, kuna utaratibu gani wa kuendeleza mpango huo kwa wananchi wanaohitaji kukopeshwa matrekta wakiwemo wananchi wa Jimbo la Manyoni Magharibi?

Supplementary Question 1

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii nami niulize maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake haya mazuri, majibu yenye kutia moyo, majibu ambayo yanaonyesha dhamira ya kweli ya Serikali katika kuondokana na dhana hii ya upungufu mkubwa wa chakula, hasa katika mikoa kame, mikoa ya katikati.
Mheshimiwa Spika, majibu yake haya yameonyesha kwamba wanakopesha vyama vya akiba na mikopo kama SACCOS. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri anasemaje juu ya wananchi wa Jimbo langu ambao wengi wao hawajajiunga na SACCOS, wataweza kupatiwa mikopo hii ya matrekta?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa Serikali imeanza kuonesha nia na wanawekeza katika kuunganisha matrekta hapa nchini, ikiwemo pale TAMCO Kibaha.
Je, katika kuwahi msimu huu wa kilimo anaweza akatutengea matrekta hata matano tu ambayo tuko tayari kuyalipia kwa awamu ya kwanza katika Jimbo la Manyoni Magharibi, Halmashauri ya Itigi?

Name

Dr. Mary Machuche Mwanjelwa

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mbeya Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba niseme kwamba katika majibu yangu ya msingi nikianzia na lile swali lake la pili nimejibu kwamba wananchi wanaweza wakajiunga katika vikundi ili waweze kukopeshwa kupitia katika Mfuko wa SACCOS. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini vilevile nikija katika swali lake la kwanza, ameuliza kama wananchi wanaweza wakakopeshwa mmojammoja. Na mimi naomba nimwambie kabisa Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi kwamba Wizara ya Kilimo imefanya utaratibu kupitia Mfuko wake wa Taifa wa Pembejeo na Kilimo, kwamba tunaruhusu mkulima yeyote mmojammoja kuweza kukopa jinsi anavyotaka.
Mheshimiwa Spika, kubwa la msingi aweze kwenda kwenye halmashauri zetu kule atakutana na maafisa wa kilimo na mkurugenzi, atajaza fomu atapeleka katika mfuko wetu wa pembejeo akiwa na proforma invoice yake na sisi kupitia mfuko huo tuko tayari hata kutoa mifuko kwa wakulima na mikopo kwa wakulima wadogo wadogo. Ahsante. (Makofi)