Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

George Malima Lubeleje

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. GEORGE M. LUBELEJE aliuliza:- Kati ya Kijiji cha Mbori na Kijiji cha Tambi upo mto ambao hujaa maji wakati wa mvua na kusababisha wananchi na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Tambi na Sekondari ya Matomondo kushindwa kuvuka:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga daraja katika mto huo ili wananchi na wanafunzi waweze kuvuka?

Supplementary Question 1

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri lakini ahadi hizi ni za muda mrefu kwamba Serikali ina mpango na mkakati wa kujenga daraja hili la Manamba kwenda Kijiji cha Tambi. Hapa anazungumzia kuhusu usanifu, je, ni lini sasa daraja hili litajengwa? Daraja hili ni upana wa mita 100 na wanafunzi wanashindwa kuvuka, ni lini sasa atajenga daraja hili?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari wanashindwa kuvuka mto huu kwenda shule ya sekondari na kwenda shule ya msingi na ni kero kubwa sana. Ni lini sasa pamoja na kutathmini mtajenga daraja hilo? Hata Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI analifahamu.

Name

Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Seneta wetu Mheshimiwa Mzee Lubeleje ambapo mimi huwa napenda kumuita grader la zamani makali yale yale. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli anayosema Mheshimiwa Lubeleje. Daraja lenyewe linaunganisha maeneo ya Mseta na Nambi lakini daraja lile ni kubwa kidogo na sasa hivi kuna korongo hata Mheshimiwa Mbunge anafahamu juzi juzi nilikuwa pamoja naye kule, ukiangalia tuna kazi kubwa ya kufanya. Tulikuwa na fedha kutoka DFID ambapo tulianza katika maeneo ili kuondoa vikwazo, tumekamilisha katika baadhi ya maeneo lakini pale lazima iwe fedha ya kutosha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika tathmini inayofanyika lengo ni kutafuta fedha kwa sababu daraja lile siyo la shilingi millioni 300 au 4000, ni daraja kubwa linalotaka zaidi ya bilioni 2. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tunalifahamu daraja hilo na nimuagize Mtendaji wetu Mkuu, watu wameshafanya design pale afike yeye mwenyewe Mhandisi Seif akaangalie ili katika mpango wa bajeti tuweke vipaumbele kwa sababu eneo lile lina watu wengi lazima tuweze kuwaokoa. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Lubeleje kwamba jambo lile tunalifanyia kazi kwa nguvu zote.

Name

John John Mnyika

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Kibamba

Primary Question

MHE. GEORGE M. LUBELEJE aliuliza:- Kati ya Kijiji cha Mbori na Kijiji cha Tambi upo mto ambao hujaa maji wakati wa mvua na kusababisha wananchi na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Tambi na Sekondari ya Matomondo kushindwa kuvuka:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga daraja katika mto huo ili wananchi na wanafunzi waweze kuvuka?

Supplementary Question 2

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Matatizo ya kukosekana kwa madaraja na kusababisha watu kushindwa kuvuka yapo vilevile kwenye Kata ya Goba hasa Mtaa wa Kulangwa na kwenye mitaa kadhaa. Kwa sababu Serikali inalifahamu suala hili na Mheshimiwa Waziri wakati anajibu swali alisema kuna fedha maalum wanazitafuta. Je, watakapotafuta fedha maalum ni pamoja na Kata ya Goba ili kwenda kuondoa matatizo ya madaraja Mtaa wa Kulangwa na mitaa mingine? (Makofi)

Name

Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la ndugu yangu Mheshimiwa Mnyika, Mbunge wa Kibamba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tunafahamu maeneo yenye changamoto mbalimbali ikiwepo katika Jimbo a Kibamba na tukifahamu wazi kwamba katika eneo la Dar es Salaam kuna maeneo mengi tumeanza kuya-address kupitia mradi wa DMDP lakini hata hivyo kuna maeneo mengine bado hasa katika Wilaya ya Kigamboni na baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Ubungo. Siwezi kutoa commitment ya moja kwa moja hapo kwa sababu mimi sitaki kuzungumza biashara ya uongo lakini kama Serikali tunaichukua changamoto hii na kuhakikisha wataalam wetu wanapitia maeneo hayo halafu kuangalia kipi kiwekwe kwenye kipaumbele cha kwanza ili kuwasaidia wananchi wetu waweze kusafiri na kutekeleza kufanya huduma zingine za kijamii. Ahsante.

Name

Dr. Mary Michael Nagu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. GEORGE M. LUBELEJE aliuliza:- Kati ya Kijiji cha Mbori na Kijiji cha Tambi upo mto ambao hujaa maji wakati wa mvua na kusababisha wananchi na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Tambi na Sekondari ya Matomondo kushindwa kuvuka:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga daraja katika mto huo ili wananchi na wanafunzi waweze kuvuka?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Kutoka Mogitu kwenda Basotu na Haydom, kuna barabara ambayo inawafikisha watu hospitali wanapougua lakini kwa bahati mbaya kutokana na mvua maji mengi kutoka ukuta wa bonde la ufa yamekuwa yakiharibu ile barabara mpaka imefungwa na watu wawili kufia pale. Je, Waziri anasema nini kuhusu barabara hii? Nitashukuru watu wa Hanang wakisikia ili wawe na moyo wa kuendelea kuishi.

Name

Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nimpongeze mama yangu Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu kwa kazi kubwa sana anayofanya katika Jimbo la Hanang. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii ni miongoni mwa barabara ambazo nimezipita mara kwa mara na nimepita mpaka Dongobesh. Ni kweli kuna changamoto kubwa na juzi juzi alinipa taarifa ya barabara hii na nyingine. Kubwa zaidi niseme siku ileile tuliyoongea niliweza kuwasiliana na Mtendaji wetu Mkuu wa TARURA kuhakikisha wanafanya tathmini ikiwa ni pamoja na barabara za Kilindi Mkoani Tanga. Imani yangu watu wangu wako site hivi sasa ama wanaelekea site ili tupate jawabu halisia nini tufanye tuweze kuwasaidia. Ni kweli najua kweli kuna changamoto katika eneo hilo. Ahsante sana. (Makofi)