Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 1 Union Affairs Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano 8 2024-01-30

Name

Omar Ali Omar

Sex

Male

Party

ACT

Constituent

Wete

Primary Question

MHE. OMAR ALI OMAR aliuliza:¬-

Je, lini Serikali itajenga ukuta wa Ikulu Ndogo ya Muungano Pemba?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Omar Ali Omar, Mbunge wa Jimbo la Wete, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imeshaandaa mipango mahususi ya kutekeleza suala hilo ambapo tathmini ya kitaalamu ya kina imefanyika ili kupata gharama za ukarabati wa Jengo la Ikulu ndogo ya Muungano Pemba ikiwa ni pamoja na ujenzi wa ukuta. Aidha, inategemewa kuwa, utekelezaji utaanza katika mwaka wa fedha 2024/2025, nakushukuru.