Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 8 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 132 2024-02-08

Name

Benaya Liuka Kapinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Vijijini

Primary Question

MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza: -

Je, ni lini Shule ya Sekondari ya Hagati itapandishwa hadhi kuwa ya kidato cha tano na sita?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Benaya Liuka Kapinga, Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ilipeleka fedha shilingi milioni 128 kwa ajili ya ujenzi wa bweni. Ujenzi umekamilika na taratibu za usajili wa kidato cha tano unaendelea. Tayari halmashauri imeomba kibali cha kupandisha hadhi ya kuwa kidato cha tano na sita, kwa barua yenye Kumb. Na. MDC/E.80/31/150 ya tarehe 15 Januari, 2024. Hivyo shule inatarajia kuanza rasmi kwa kidato cha tano na sita Julai, 2024.