Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 12 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 199 2024-02-14

Name

Anna Richard Lupembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nsimbo

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:-

Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji katika Kata ya Urulwa, Kijiji cha Usense – Nsimbo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Anna Richard Lupembe, Mbunge wa Nsimbo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa Mradi wa umwagiliaji wa Usense ulianza mwaka wa fedha 2021/2022 na ujenzi huu ulikusudiwa kukamilika baada ya miezi sita. Hata hivyo, ujenzi wa miundombinu katika skimu hii haukukamilika kutokana na mkandarasi kushindwa kutekeleza kazi kulingana na mkataba hali iliyopelekea mkataba kusitishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetangaza upya zabuni ya mradi huo ili kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika Skimu ya Usense. Mchakato wa manunuzi utakapokamilika, ujenzi utaanza mara moja. Kukamilika kwa mradi huu kutanufaisha wakazi wa Vijiji vya Usense, Ururwa na Ikondamoyo.