Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Anna Richard Lupembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nsimbo

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji katika Kata ya Urulwa, Kijiji cha Usense – Nsimbo?

Supplementary Question 1

MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini mkandarasi huyu ambaye alikuwepo kwenye Skimu ya Usense hakushindwa kujenga skimu ile ila pesa hakuweza kupatiwa kwa wakati na tukakatisha mkataba wake na Sasa hivi tupo kwenye mchakato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na uzoefu wa skimu zingine kama kwenye Jimbo langu kuna Skimu ya Ughala ilikuwa hivyo hivyo tulipoteza bilioni moja na sasa tumepata hofu kupitia hii skimu; je, kutokana na huo mchakato mpaka sasa hivi umechukua muda mrefu takribani miaka miwili, ni lini utakamilika na lini ujenzi utaanza mara moja?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; kutokana na wananchi wanahamu ya kulima kupitia skimu hii ambayo mlitupangia takribani milioni 700; je, kutokana na ucheleweshaji Mheshimiwa Waziri yupo tayari kwenda na mimi kuhakikisha na kuona uhalisia wa hizi skimu zote mbili, Skimu ya Usense pamoja na Ughala?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Jambo la kwanza nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Nsimbo kwamba mradi wake kama ambavyo ipo katika mchakato, hii mchakato tuliopo sasa hivi wa upembuzi yakinifu, ninaamini tutaumaliza kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha na mradi huu tutauweka katika mwaka wa fedha unaokuja ili uanze utekelezaji wake ili wananchi wa Jimbo la Nsimbo waweze kupata hiyo faida lakini kwenda na yeye nipo tayari muda wowote tukashuhudie hicho ambacho Mheshimiwa Mbunge amekieleza.

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji katika Kata ya Urulwa, Kijiji cha Usense – Nsimbo?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wananchi Kata ya Ruaha Mbuyuni waliopo katika Wilaya ya Kilolo wanapata shida sana kwa sababu mradi wao wa umwagiliaji, mto ulichepuka, lakini wana Mradi wa Umwagiliaji ule wa Mgambalenga toka 2014 bado wanateseka. Je, ni lini sasa mateso hayo yataisha kwa Wananchi wa Kata ya Ruaha Mbuyuni?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Mradi wa Gambalenga ni miongoni mwa miradi ambayo Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imepanga kupeleka maboresho makubwa. Kwa hiyo, tunachokifanya sasa ni upembuzi yakinifu ili tuende tukaurekebishe ili wananchi wa eneo hilo waweze kufaidika.

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji katika Kata ya Urulwa, Kijiji cha Usense – Nsimbo?

Supplementary Question 3

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, mwaka jana Serikali kupitia Wizara ya Kilimo ilipitisha bajeti ya kufanya visibility study kwenye Skimu ya Makersho, Metrom, Kikafu chini, Bolutu, Longoi A-B, kimashuku lakini pamoja na mifereji mingine. Ni lini sasa Serikali itaanza kufanya visibility study na kujenga hizi skimu?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Tume ya Umwagiliaji inaendelea na kazi ya usanifu na upembuzi wa kina wa miradi karibu 100 nchini ikiwemo Miradi ya Makeresho, Kikapuchini na mingine ambayo Mheshimiwa Mbunge ameitaja. Kwa hiyo, tukishamaliza hayo tutakwenda katika hatua ya pili ya kutafuta mzabuni baada ya hapo ni utekelezaji wa mradi wenyewe. Kwa hiyo, tupo katika hiyo hatua katika mwaka huu wa fedha, ahsante. (Makofi)