Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 4 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 114 2023-11-08

Name

Yahaya Omary Massare

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Magharibi

Primary Question

MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza: -

Je, lini Tume ya Umwagiliaji itatimiza ahadi yake ya kuvuna maji ya mvua katika Mbuga inayozunguka Mji wa Itigi ili kuepusha mafuriko?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yahaya Omary Massare, Mbunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu spika, katika Mwaka wa Fedha 2023/24, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya imetenga fedha kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili kuweza kuchimba na kujenga mifereji ya kuongoza maji kutoka bonde linalozunguka Mji wa Itigi na kuelekeza maji hayo mashambani.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, utekelezaji wa ujenzi wa mifereji hiyo utasaidia kuepusha mafuriko yanayojitokeza katika Mji wa Itigi.