Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 14 | Sitting 13 | Defence and National Service | Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa | 224 | 2024-02-15 |
Name
Cecil David Mwambe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ndanda
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:-
Je, kweli kuna wazee wanaodai haki zao kutokana na ushiriki wao kwenye Vita vya Dunia au Jeshi la KAR?
Name
Dr. Stergomena Lawrence Tax
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nominated
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI K.n.y. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cecil David Mwambe, Mbunge Ndanda, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba wapo wazee waliopigana Vita ya Pili ya Dunia (1939 - 1945) wakiwa askari wa Jeshi la KING’S AFRICAN RIFLES (KAR) lililokuwa chini ya Serikali ya Kikoloni ya Uingereza. Haki wanazodai zinahusiana na mali walizoachiwa na Serikali ya Uingereza mara baada ya utawala wao Tanganyika kukoma.
Mheshimiwa Spika, nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved